UVCCM yalaani maandamano, vurugu Oktoba 29

By Pilly Kigome , Nipashe Jumapili
Published at 03:27 PM Nov 09 2025
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Tanzania(UVCCM), Mohamed Kawaida
PICHA: PILLY KIGOME
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Tanzania(UVCCM), Mohamed Kawaida

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Tanzania(UVCCM), Mohamed Kawaida ametoa rai kwa wana siasa wa vyama vyote nchini ikiwemo CCM kuacha maneno ya kejeli na matamko yenye kuleta taharuki au kuligawa Taifa.

Rai hiyo ameitoa leo Novemba 9, 2025 jijini Dar es Salaam katika mkutano na waandishi wa habari. Kawaida amewataka wanasiasa hao wachunge kauli zao kwakuwa maneno hubomoa na hayajengi.

Aidha amewaomba vijana nchini kuacha vitendo viovu vya kufata mihemko ya mitandao ya kijamii wenye nia ovu na nchi hii kuingia kwenye mikumbo ya kufanya fujo na kusababisha maafa na vifo ambavyo havikuwa vya lazima.

"Nawaomba vijana wenzangu kabla ya kufanya matendo ovu  wakumbuka wagonjwa hospitalini, wakumbuke wazee na hata wajawazito waliopo nchini" amesema

Amesema vitendo  hivyo vilivyofanywa na vijana wa ndani na wengine kutoka nje ya nchi  vimeharibu na kusababisha maafa makubwa ikiwemo kuharibu miundombinu shughuli za usafirishaji katika biashara za kikanda katika miji mikubwa nchi jirani Zambia, Rwanda,Burundi Uganda Kenya waliokuwa wanategemea bandari ya Tanzania na kuharibu shughuli za kiuchumi.

"Naomba vijana tushikamane na amani na turithishe amani kwa kizazi kijacho kwakuwa amani ndio inafungua milango ya kiuwekezaji nchini tusiharibu amani na amani sio udhaifu ni nguvu inayofanya kuwe na amani endelevu naTaifa bora" amesema Kawaida

Wakati huohuo amewaomba wazazi na viongozi wa dini kwa pamoja waendelee⁹ kuwajenga vijana ili kuijenga Tanzania yenye amani na maendeleo yenye uchumi thabiti.
Pia amemponheza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuchaguliwa kuwa Rais kwa tikeki ya Chama cha Mapinduzi kukiongoza taifa kwa awamu ya sita.