MFUKO wa Taifa la Hifadhi wa Jamii (NSSF), unatarajia kujenga jengo la kitega uchumi la hoteli yenye hadhi ya nyota tano katika eneo la Njedengwa jijini Dodoma ili kuchochea uchumi na utalii mkoani humo.
Mradi huo utaanza rasmi kujengwa Mei mwakani na takriban Sh.Bilioni 148.4 zitatumika kwenye ujenzi huo.
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba ameyasema hayo leo jijini Dodoma kwenye upandaji wa miti eneo la Njedengwa ambalo litajengwa kitega uchumi hicho.
Anesema hatua hiyo ni utelekezaji wa agizo la Rais Samia Suluhu Hassan la kuwekeza majengo ya kitega uchumi katika Mkoa wa Dodoma na kwamba jengo hilo la hoteli litakuwa la ghorofa 16 na faida ya uwekezaji huo italipa ndani ya miaka 11.
Naye, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule amesema uwekezaji huo utafungua fursa za mikutano mikubwa na kuchochea ukuaji wa uchumi huku Meneja Usimamizi wa Miradi NSSF, Mhandisi Helmes Pantaleo akisema jengo hilo litakuwa ni refu kuliko yote yaliyopo Dodoma.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED