Polisi: Punguzeni wazee kwenye malindo

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 06:11 PM Jul 18 2025
Mkuu wa Polisi Jamii Mkoa wa Morogoro ACP Samuel Kijanga.
Picha: Mpigapicha Wetu
Mkuu wa Polisi Jamii Mkoa wa Morogoro ACP Samuel Kijanga.

Mkuu wa Polisi Jamii Mkoa wa Morogoro ACP Samuel Kijanga amewataka wamiliki wa kampuni za ulinzi kuajiri vijana wenye Nguvu badala ya wazee ili kuwa na ufanisi malindoni

ACP Kijanda ameyasema hayo Julai, 18, 2025 alipokutana na wamiliki wa kampuni za ulinzi wa Manispaa ya Morogoro wapatao 23 katika ukumbi wa mikutano wa JKT Umwema 

Amesema, Mazoezi na mafunzo ya mara kwa mara yafanyike ili kuweza kuzuia au kupambana na wahalifu watakaojaribu kufanya uhalifu kwenye maeneo wanayoyalinda ili mali na jamii inayowazunguka kuwa salama, lakini pia kuwashauri wateja wao kufunga kamera kwaajili ya kutunza kumbukumbu za uhalifu unapotokea ili isaidie kwenye upelelezi.

Kwa upande wake, Lukas Kaberenge mmiliki wa Kampuni ya Quick Security amesema elimu na maelekezo waliyoyapata yanaenda kuwabadilisha na kuendesha Kampuni Kisasa kuendana na hali halisi ya maisha ya sasa.