Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, amesema kiongozi asiyegusa na kero za wananchi hatoshi katika nafasi yake.
Akizungumza katika mpaka kati ya Mkoa wa Manyara na Arusha, tayari kwa kuanza ziara yake jijini Arusha baada ya kuhitimisha Manyara, aliwakumbusha viongozi wajibu huo katika uongozi.
Aliwashukuru viongozi wa jiji la Arusha kwa kwenda kumpokea tayari kwa ziara yake mkoani humo na kuwaeleza wapo tayari kufanya kazi katika mkoa huo.
“Wananchi wote mliokuja kushirikiana nasi hapa, tunaashukuru sana, niwahakikishe Chama Cha Mapinduzi kimeendelea kusimamia serikali zake kuona zinahudumia wananchi kwa upendo,” anasema.
Pia amesema hawatasita kuhangaika na kero zao kwa kuwa ndiyo msingi wa wao kuwapo kwenye nafasi.
“Kero za wananchi ni kero zetu, matatizo ya wananchi ni matatizo yetu
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED