MAHAKAMA Kuu nchini Kenya, imeondoa amri iliyokuwa inazuia Naibu Rais Mteule Kithure Kindiki kuapishwa.
Jopo la majaji watatu liliongozwa na Jaji Eric Ogola na Fredah Mugambi limetoa maagizo hayo hii leo.
Naibu wa Rais aliyeondolewa madarakani Rigathi Gachagua,alikuwa amewasilisha ombi mahakamani kuzuia mrithi wake kuchukuwa rasmi wadhifa wake.
Majaji waliendelea kutoa uamuzi kwamba kesi hiyo itatajwa Novemba 7, 2024, na kuongeza kuwa Gachagua yuko huru kuwasilisha rufaa dhidi ya uamuzi huo.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED