MAHAKAMA Kuu Nchini Kenya imetoa amri ya kusitisha utekelezaji wa azimio na Seneti na uteuzi wa Naibu Rais mpya hadi Oktoba 24 ambako suala hilo litatajwa mbele ya jopo la majaji watakao teuliwa na Jaji Mkuu Martha Koome.
Mahakama Kuu imeweka zuio la muda dhidi ya uamuzi wa Seneti wa kuunga mkono kumwondoa Naibu Rais Rigathi Gachagua leo Oktoba 18 kupitia taarifa yake chini ya Jaji Chacha Mwita.
Wakiweka zuio hilo lililotolewa na Mahakama imetaja maswali muhimu ya katiba na maslahi ya umma juu ya mchakato huo kujadiliwa na kutolewa uamuzi na jopo la majaji.
“Kwa sababu ya masuala yaliyoibuka katika ombi na maombi, na dharura iliyoonyeshwa, maagizo ya kihifadhi yanayotakiwa kuzuia utekelezaji wa uamuzi wa seneti kuhusu mashtaka ya kumuondoa Naibu Rais wa Kenya, pamoja na uteuzi wa mrithi wake, hadi tarehe 24 Oktoba 2024...” ilisomeka kwenye taarifa.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED