Watoto wabainika kutopata chanjo tangu wazaliwe

By Vitus Audax , Nipashe
Published at 07:13 PM Dec 07 2024
Mratibu wa huduma za chanjo wilayani Sikonge, mkoani Tabora, Muku Mbaga.

MRATIBU wa huduma za chanjo wilayani Sikonge, mkoani Tabora, Muku Mbaga amesema wapo watoto ambao hawajawahi kupata chanjo tangu wamezaliwe kutokana na mazingira wanayoishi kuwa na miundombinu isiyo rafiki kufikia huduma hiyo.

Mbaga amebainisha hayo wakati wa zoezi la utoaji wa chanjo kwa watoto zaidi ya 4,000  wilayani humo waishio maeneo ya vijijini ambapo kuna tatizo la miundombinu barabara.

Lengo la zoezi hilo ni kuhakikisha watoto wanalindwa dhidi ya magonjwa mbalimbali ikiwemo kifua kikuu, polio na surua.

Meneja Mradi wa Mwanzo Mwema Dk.Michael Luvanda amesema wameanzisha huduma ya Chanjo Mkoba ili kuwafikia watoto na mabinti waishio maeneo ya pembezoni na kuhakikisha huduma hiyo inawafikia wote0.

Baadhi ya Wazazi na walezi kutoka Kata za Kiloli,Kitunda na Kipili. wamesema mradi wa Mwanzo mwema unaotoa chanjo mkoba kwa kushirikiana na serikali umekuwa suluhu ya ukosefu wa huduma za chanjo katika maeneo yao.