Mwanamke aliyehisi hana wazazi halisi, awasaka kimtandao, awapata ‘uso kwa uso’

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 12:28 PM Dec 19 2024
Ni simulizi ya aina yake, panaposhuhudiwa utashi na mshangao, mwanamama mwenye umri wa kati kutoka Marekani, Tamona Mosridze, amehisi wazazi wake sio sahihi, pia historia ya maisha yake.
Picha: Mtandao
Ni simulizi ya aina yake, panaposhuhudiwa utashi na mshangao, mwanamama mwenye umri wa kati kutoka Marekani, Tamona Mosridze, amehisi wazazi wake sio sahihi, pia historia ya maisha yake.

Ni simulizi ya aina yake, panaposhuhudiwa utashi na mshangao, mwanamama mwenye umri wa kati kutoka Marekani, Tamona Mosridze, amehisi wazazi wake sio sahihi, pia historia ya maisha yake.

Akiwa na mawazo hayo, akadodosa dalili za ukweli ulioko, pale anawapopiga simu anayemhisi ndiye ana aina ya majibu yanayomfikia.

Dodosa yake ni kumpata mwanamke mama yake halisi. Kwake, mawazo hayo yakaonekana kama ndoto.

Tamona anasimulia: “Kilichomshangaza ni ile hali ya ubaridi na hasira ya yule mwanamke wa upande wa pili wa simu, ananitamkia kwa kelele, hata kufikia kulia... ‘sijawahi kupata mtoto na sitaki kuzungumza nami...

"Majibu yake yalinishangaza zaidi kuliko alivyonikasirisha. Nilikuwa tayari kwa lolote, lakini majibu yake yalikuwa zaidi ya vile ambavyo ningeweza kufikiria."

Tamona, mwenye umri wa miaka 40, sasa analitafsiri hilo tukio la Agosti mwaka huu, huenda mhusika hapendi kuhusishwa na hayo maishani mwake. 

Lakini Tamona hakukata tamaa kirahisi, akataka kujua jinsi alivyolelewa, baba yake ni nani, siri ambayo mama yake ndiye pekee anaweza kuifafanua.

Wakati ni hatua hiyo kufikiwa, lakini Tamona alianza kumtafuta mama huyo mnamo mwaka wa 2016, pale alipokuwa anasafisha nyumba ya mama yake.

Hapo akashangaa kupata cheti cha kuzaliwa, jina la Tamona likaandikwa kwenye nyaraka hiyo, lakini tarehe yake ya kuzaliwa hakuamini ilikuwa sahihi.

Hiyo ikamfanya ashuku kuwa anaweza kuwa ‘mtoto wa kulelewa’ na baada ya kufanya utafiti, akaanzisha kikundi cha mtandao wa ‘facebook’ ikisomeka kwa Kiingereza "I'm Looking,"(ninamtafuta) kwa matumaini ya kupata wazazi wake halisi.

Pia, akafichua ulanguzi wa watoto ulioko huko Georgia, Marekani, akitaja inabadilisha maisha ya mamia ya watu. 

Kwa miongo kadhaa wazazi walidanganywa, wakidai watoto wao wamekufa wakiwa, kumbe wanauzwa.

Tamona, ambaye kitaaluma ni mwandishi wa habari kupitia mtandao huo akaunganisha mamia ya familia kupitia kazi yake, lakini binafsi hakufichua siri ya maisha yake ya zamani, siri yake akiamini, huenda ametekwa nyara akiwa mtoto.

"Nilikuwa nashughulikia kesi hii kama mwandishi, lakini pia ilikuwa kusudio langu binafsi," anasema.

Hapo akaaanza msako na kupokea ujumbe kupitia ukurasa wake wa ‘facebook’, ndio pale mmoja anayeishi vijijini vya Georgia, akamfahamisha kumjua mwanamke aliyemficha ujauzito wake na alijifungua huko Tbilisi mnamo Septemba, 1984.

Ni tarehe ya kuzaliwa ambayo mtu, iliyolingana na  ile ya Tamona aliyoichapisha kwenye mitandao ya kijamii; mwanaume huyo aliamini kuwa mwanamke huyu ndiyo mama yake Tamona, huku akimpa Tamona hata jina lake halisi.AMGUNDUA SHANGAZI YAKE

Tamona akaanza mara moja kumtafuta mtandaoni, lakini hakuweza kumpata, hata akaamua kutuma ombi kwenye mtandao wa ‘Facebook’ kuwauliza kuwapo  anayemfahamu.

Mwanamke mmoja akajibu haraka kwamba mwanamke aliyeficha ujauzito wake ni shangazi yake, lakini akamwomba Tamona aondoe chapisho hilo na akakubali kupimwa DNA.

Wakiwa wanasubiri majibu ya DNA, Tamona aliwasiliana na mama yake.

Wiki moja baadaye, matokeo ya DNA yakatoka kwa kuthibitisha Tamona na mwanamke huyo kwenye Facebook walikuwa mabinamu. 

Kwa ushahidi huo, Tamona akaamua kumshawishi mama yake kukiri ukweli na kufichua jina la baba yake, ndipo akapatiwa, lilikuwa Gorgon Khoruwa.

"Miezi miwili ya kwanza ilikuwa ya kushangaza," anasema na kuongeza: "Sikuamini haya yote yaliyokuwa yakitokea. Sikuamini kuwa nilikuwa nimewapata."

Baada ya kupokea jina hilo la baba, Tamona akampata haraka kwenye mtandao  wa ‘facebook’ akibaini ni mfuasi wake Tamona kwenye mtandao huo wa kijamii. 

Leo hii, kazi ya Tamona katika kuunganisha familia sasa inajulikana sana kote nchini Georgia, akiwa kwenye orodha ya marafiki zake kwa miaka mitatu; awali Gorgon hakujijua kuwa sehemu ya hadithi ya Tamona.

Wakapanga kukutana haraka huko Zugdidi, Magharibi mwa Jimbo la Georgia alikozaliwa, umbali wa kilomita 260 kutoka nyumbani kwa Tamona huko Tbilisi.

Sasa Tamona, anakumbuka siku za nyuma hilo lilimshtusha sana, leo hii lina mvuto.

Kimsingi, mama huyo akaanza kumsaka na mzee huyo mwenye umri wa miaka 72 na alipofika kukutana naye, akisimulia walikumbatiana kwa furaha, kisha wakasimama kwa muda kutazamana kwa tabasamu.

Tamona anasimulia: "Ilikuwa ajabu, aliponitazama, alijua mimi ni binti yake. Tulikuwa na hisia mseto sana."

Lakini bado moyoni, Tamona akawa na maswali mengi na hakujua pa kuanzia, akidokeza: "tuliketi tu, tukatazamana na kujaribu kutafuta pa kuanzia."

WAMEFANANA SANA

Walipokuwa wakizungumza, anasema akagundua kwamba walikuwa na mengi ya kufanana.

Gorgan, wakati mmoja alikuwa mcheza dansi maarufu huko Georgia, pia alifurahi kwamba Tamona (wajukuu zake) walipenda kucheza hivyo.

"Binti zangu wote wawili wanapenda kucheza dansi, pia mke wangu," anasimulia na kucheka.

Gorgon akaialika familia yake yote nyumbani kuonana na Tamona, hata akawatambulisha kwa kundi kubwa la jamaa zake; akikutana na kaka na dada zake, wajombae, wanawe na wakwe zake.

Kila mtu katika familia akakubali Tamona anafanana sana na baba yake, mwenyewe anayefananishwa, akiunga mkono kwa hoja "kati ya watoto wake wote, nilifanana zaidi na baba yangu."

Hapo wakatumia jioni hiyo, kukumbuka mambo yaliyopita, kula chakula chao kimila, wakaimba nyimbo za kikwao - Georgia na kucheza huku  wakipiga kinanda maalum.

SWALI LILOBAKI 

Swali moja bado lilibaki akilini mwake Tamona, kama je, alitekwa nyara kutoka kwa mama yake wakati wa kuzaliwa, au aliuzwa? 

Kwa kuwa baba na mama yake walezi wamekufa, akashindwa kupata majibu na hatimaye, mwezi Oktoba uliyopita, Tamona akapata fursa ya kumuuliza uhalisia wa mama yake ni nani.

 Kituo cha televisheni cha Poland kilikuwa kikitengeneza filamu kuhusu Tamona na kumpeleka kukutana na mama yake. Mama yake akakubali kuongea naye faragha.

MZIZI WAKE KUZALIWA

Tofauti na watu wengi ambao Tamona akawasaidia kuungana na familia zao, akagundua kwamba hakuwa ametekwa nyara akiwa mtoto. 

Ni kwamba mama yake alikuwa amemwacha na kuficha siri hiyo kwa miaka 40 na wazazi wake hawakuwa na uhusiano, bali walikuwa pamoja kwa muda mfupi tu. 

Mama yake akaona aibu sana wakati huo na kuamua kuficha ujauzito wake mnamo Septemba 1984, aliposafiri kwenda eneo la Tibilisi, kwa kisingizio cha upasuaji.

Ukweli ni kwamba, binti yake alibaki huko hadi mchakato wa kuasili wa Tamona ulipokamilika.

"Nilipogundua kuwa nimechukuliwa na mtu mwingine na nilikuwa nimekaa kwa siku kumi tu na mama yangu, nilihisi uchungu sana," Tamona anasema kwa huzuni, akinena "ninajaribu kujizuia kufikiria hilo."

 Sasa, anaamini si haki kwa kinamama na baba, kuwa na nyendo kama hizo za watoto wao kupotoshwa.

Sasa anafafanua, uhalisia penye udanganyifu wa aina hiyo, ni ngumu kuwapo atakayeamini uhalisia wa upotoshaji wa kinamama kwa aina hiyo.

Baadaye, mama yake akamwomba aondoke nyumbani na hawakuzungumza tena baada ya hapo.

Leo hii anasema: "Je, niko tayari kupitia hatua hizi zote tena? Kwa kweli, ndivyo nilivyofanya, nilijifunza mengi kuhusu familia yangu mpya."

 BBC