Katika orodha ya kila mwaka ya familia tajiri zaidi ulimwenguni ambayo huandaliwa na Bloomberg, familia ya Walton, mmiliki wa maduka makubwa nchini Marekani Walmart, ilishika nafasi ya kwanza mnamo 2024.
Miongo sita baada ya Sam Walton kufungua duka kuu la kwanza huko Arkansas, warithi wake ni matajiri zaidi kuliko hapo awali kutokana na utendaji uliovutia wawekezaji wa hisa za kimataifa, ambazo thamani yake imeongezeka kwa asilimia 80 mwaka huu.
Siri mojawapo ni kampuni zinazounda orodha hiyo, kwa mujibu wa Bloomberg, ni kwamba zimeendelea kuwa na umoja katika umiliki wa mali zao na, wakati fulani, zimeunda makubaliano ya kibiashara ambayo yanasimamia kuunganisha utajiri wao.
Familia nyingi katika orodha ya mwaka huu, kwa mujibu wa Bloomberg, zimekuwa tajiri zaidi kutokana na faida kubwa iliyorekodiwa kwenye soko la hisa.
FAMILIA TAJIRI DUNIANI
1. Familia ya Walton;
Utajiri wake Ni Dola za Marekani bilioni432 .Walton wanamiliki takriban 46% ya maduka makubwa, hisa ambayo ni msingi wa utajiri mkubwa wa familia hiyo.
Mwanzilishi wake, Sam Walton, aligawanya mali kati ya watoto wake kimkakati ili kuimarisha uchumi wa familia.
Unaweza pia kusoma:
2. Familia ya Al Nahyan:
Wana Dola za Marekani bilioni 323,
Katika Umoja wa Falme za Kiarabu, familia tawala ya Al Nahyan ilizalisha utajiri wake kutokana na biashara ya mafuta.
Mtawala wa Abu Dhabi (mmoja kati ya wafalme saba), Shekhe Mohammed bin Zayed Al Nahyan, pia ni rais wa nchi hiyo.
3. Familia ya Al Thani:
Utajiri wao Dola 172 bilioni na wanaishi Qatar.
Serikali ya familia ya Al Thani nchini Qatar ina maslahi ya kibiashara katika sekta ya mafuta na gesi.
Wanafamilia wanashikilia nyadhifa maarufu za kisiasa na wanamiliki kampuni kubwa katika tasnia mbalimbali.
Familia ni kubwa, ingawa nguvu yake kiuchumi imejilimbikizia katika maeneo machache muhimu.
4. Familia ya Hermes:
Pesa zao ni Dola za Marekani 170 bilioni na wanaishi Ufaransa, wanamiliki kampuni ya mitindo ya kifahari nchini Ufaransa.Miongoni mwa wanafamilia wanaoshikilia nyadhifa za utendaji katika kampuni hiyo ni Axel Dumas, Mkurugenzi Mtendaji.
5. Familia ya Kochs:
Utajiri wao Dola bilioni 148. Ndugu Frederick, Charles, David na William Koch walirithi kampuni ya mafuta kutoka kwa baba yao, Fred. Lakini baada ya msuguanoo, ni Charles na David pekee waliobaki kwenye biashara hiyo.
Kampuni ya Koch ina biashara katika mafuta ya petroli, kemikali, nishati, madini, teknolojia ya komputa, fedha, biashara ya bidhaa, uwekezaji, miongoni mwa nyingine.
6. Familia ya Al Saud:
Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman ni sehemu ya familia. Sekta yao ni viwanda wakiwa na utajiri wao Dola za Marekani bilioni 850.
Utajiri wa familia ya Kifalme wa Saudia.
7. Familia ya Mars:
Utajiri wao ni Dola bilioni 133, wakimiliki kampuni ya Mars inayojulikana kwa bidhaa zake kama vile biskuti za chokoleti maarufu, ingawa bidhaa za utunzaji wa wanyama sasa zinachangia zaidi ya nusu ya mapato ya kampuni hiyo.
8. Familia ya Ambani:
Wana kampuni ya Reliance Industries
yenye utajiri wa Dola bilioni 99 nchini
India. Mukesh Ambani ndiye anayesimamia eneo kubwa zaidi la kusafisha mafuta duniani.
Anaishi katika jumba la ghorofa 27 huko Mumbai, linalotajwa kuwa makazi binafsi ya gharama kubwa zaidi ulimwenguni. Yeye na kaka yake walirithi mali kutoka kwa baba yao.
Familia hiyo iliangaziwa hivi karibuni katika harusi ya Mukesh Ambani na Radhika Merchant. Ndoa hiyo ilitanguliwa na miezi minne ya matukio ya kifahari, ikiwa ni pamoja na matamasha ya nyota wa pop kama Rihanna.
9. Familia ya Wertheimer:
Utajiri: Dola za Marekani bilioni 88 nchini Ufaransa na wanandugu Alain na Gerard Wertheimer walirithi utajiri ambao babu yao aliyebuni ufadhili Coco Chanel huko Paris katika miaka ya 1920.
Familia yake inamiliki jumba la mitindo na pia farasi wa mashindano na mashamba ya mizabibu.
10. Familia ya Thomson:
Utajiri: Dola za Marekani bilioni 87 huko nchini Canada.Familia inamiliki takriban 70% ya hisa katika data na huduma za kifedha kutoka Thomson Reuters.
Utajiri wa familia tajiri zaidi ya Canada ulianza mapema miaka ya 1930 wakati Roy Thomson alifungua kituo cha redio huko Ontario.
Kwa mujibu wa BBC
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED