MKULIMA wa mazao ya bustani kutoka mkoani Manyara, Shaban Manota, anatarajia kuzindua mifumo ubunifu kiteknolojia katika kilimo, ili kusaidia kutoa elimu katika maonesho ya kimataifa ya wakulima Nanenane.
Mifumo anayozindua ni Mfumo Jumuishi wa Kilimo na Mfumo Jumuishi wa Mazao ya Kilimo, utakaosaidia wakulima kuepuka hasara kipindi cha mavuno.
Akizungumza na waandishi wa habari katika maonesho hayo, kwa miaka mingi wakulima wamekuwa wakilima bila kumbukumbu kutokana na kukosekana kwa mifumo.
Amesema mifumo hiyo itawasaidia wakulima kulima kilimo chenye tija lakini pia mifumo hiyo imezinduliwa, ili kuunga mkono jitihada za serikali za kuleta mabadiliko katika sekta ya kilimo.
Amesema kupitia mifumo huo, utawezesha maofisa ugani, wauzaji wa pembejeo (agrovets), wasindikaji, taasisi za fedha na serikali, kushirikiana kwa karibu, ili kuhakikisha wakulima wanapiga hatua.
Amesema mafanikio hayo yanatokana na mpango wa Jenga Kesho iliyobora (BBT), kupitia mradi wa ICT in Agriculture, kwa kushirikiana na serikali.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED