Wataalam wa Wizara ya Maliasili na Utalii kutoa Elimu ya Uhifadhi Simiyu

By Mwandishi Wetu , Nipashe Jumapili
Published at 09:13 AM Oct 05 2025
Wataalam wa Wizara ya Maliasili na Utalii kutoa Elimu ya Uhifadhi Simiyu
Picha: Mpigapicha Wetu
Wataalam wa Wizara ya Maliasili na Utalii kutoa Elimu ya Uhifadhi Simiyu

Baadhi ya wajumbe wa Timu ya Wataalam kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii wamewasili mkoani Simiyu kwa ajili ya kutoa elimu ya uhifadhi kwa jamii.

Elimu hiyo inalenga kuwawezesha wananchi kujikinga na wanyama wakali na waharibifu,Taratibu na kanuni za kumiliki Nyara za Serikali pamoja na kuimarisha mahusiano kati ya jamii na mamlaka za hifadhi.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Prisca Kayombo, amepokea rasmi timu hiyo ya wataalam jana Oktoba 04,2025 tayari kuanza utekelezaji wa majukumu yao mkoani humo.

Timu hiyo ya elimu kwa jamii inaundwa na wataalam kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Idara ya Wanyamapori, Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori - TAWA pamoja na maafisa Wanyamapori kutoka halmashauri husika.

Zoezi la utoaji elimu hiyo litafanyika katika maeneo yenye changamoto kubwa za wanyama wakali, hususan fisi waliouawa hivi karibuni katika Wilaya za Busega na Itilima.