Mgombea Mwenza wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk.Emmanuel Nchimbi bado yupo mkoani Tabora ambako anaendelea na kampeni za kunadi sera za chama hicho pamoja na kuomba kura kuelekea Uchagzi Mkuu Oktoba 29 mwaka huu.
Dk.Nchimbi katika kampeni hizo anaendelea kuipeperusha bendera ya chama hicho akinadi sera na kuwanadi wagombea katika maeneo yote anayopita akiwemo Mgombea Urais wa CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Kwa mujibu wa ratiba ya kampeni hizo, Dk. Nchimbi leo Oktoba 05, 2025 atafanya mikutano miwili ambapo ataanza na mkutano Sikonge kwenye Uwanja wa TASAF na kisha atamaliza siku yake kwa mkutano mkubwa utakaofanyika Kaliua kwenye Viwanja vya Konane.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED