Mgombea Urais Kupitia Chama Cha NLD Doyo Hassan Doyo, amesema akishinda katika nafasi hiyo atatumia rasilimali zilizopo kuleta maendeleo.
Doyo ameyasema hayo jana akiwa mkoani Mara katika mwendelezo wa safari yake ya kusaka kura za kushinda kiti cha Urais. Ameahidi akishinda atatenga bajeti ya kujenga maeneo ya wazi ya serikali kwaajili ya kuleta vivutio vya utalii katika Mji wa Mugumu na atawakopesha wafanyabiashara fedha ili wajenge Majengo ya kisasa kwaajili ya kupokea wageni katika sekta ya utalii.
Aidha amesema atahakikisha barabara zinazotoka Serengeti kwenda Arusha, Bunda, Tarime, Musoma serikali yake itazijenga kwa kiwango cha zege ili ziweze kupitika kila msimu. Aidha Doyo amehoji Mkoa wa Mara ndio unaoongoza kwa kuwa na madini mengi nchini lakini kwanini watu wake wana maisha magumu na wananyanyasika kila kukicha na kwamba wakimchagua yeye itakuwa mwisho wa wao kupitia Hali hiyo.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED