UDP kujenga viwanda kila mkoa

By Paul Mabeja , Nipashe Jumapili
Published at 03:47 PM Sep 21 2025
Mkalimani wa lugha ya alama Joseph Paul kushoto akitoa tafsiri ya hotuba ya mgombea urais kupitia Chama cha UDP Saum Rashid, leo jijini Dodoma kwa baadhi ya watu wenye ulemavu wa kutosikia (viziwi)
PICHA: MPIGAPICHA WETU
Mkalimani wa lugha ya alama Joseph Paul kushoto akitoa tafsiri ya hotuba ya mgombea urais kupitia Chama cha UDP Saum Rashid, leo jijini Dodoma kwa baadhi ya watu wenye ulemavu wa kutosikia (viziwi)

MGOMBEA urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha UDP, Saumu Rashid, amesema kama Watanzania watampa ridhaa ya kuongoza nchi kwenye uchaguzi mkuu mwaka huu atahakikisha anajenga kiwanda kila mkoa kulingana na rasilimali zilizopo.

Alisema hayo leo wakati akihutubia wakazi wa kata ya Chang'ombe jijini Dodoma kwenye mkutano wa kampeni kwa ajili ya Chama hicho kunadi sera zake. "Katika sekta ya viwanda tutahakikisha tunajenga kiwanda kila mkoa kulingana na rasimali zilizopo mkoa husika sera yetu ni  kuwajaza mapesa Watanzania, hivyo lazima tufungue fursa za uchumi ili kila mtanzania anufaike",amesema 

Amesema pia watahakikisha wanakuza zao la zabibu katika mkoa wa Dodoma ili wananchi wanufake nalo kwa kuanzisha viwanda vya uzalishaji mvinyo kwa ajili kuuza ndani na nje ya mipaka nchi.Amesema hivi sasa wakulima wa zao hilo bado hawanufaiki nalo kutokana na kukosekana kwa viwanda vya kutosha vya uzalishaji wa mvinyo na kusabanisha kiasi kikubwa mazao kuharibika yakiwa shambani.

"Tumedhamilia kupata wataalam wa kutosha kuboresha miundomubinu ya kilimo pamoja na kupima udongo ili kukuza kipato chetu,"amesema kipaumbele kingine ni sekta ya Afya ambapo wataanzisha mfumo wa huduma za afya kwa wote bila kujali itikadi ya mtu.