Balozi wa India nchini Tanzania, Bishwadin Dey amesifia kukua kwa uhusiano wa Tanzania na India akisema kiwango cha biashara baina ya nchi hizo kimeongezeka hadi kufikia kiasi cha dola bilioni 8.6 mwaka 2024/25.Huku uwekezaji wa India kwa Tanzania ukifikia dola bilioni 5.
Balozi Dey alisema hayo wakati wa kutoa zawadi kwa wachoraji bora katika mashindano ya uchoraji yaliyoandaliwa na ubalozi wa India nchini kwa kushirikiana na shule kumi maarufu zaidi za Dar es Salaam.
“Tanzania kwa sasa ndio mshirika wa pili kwa ukubwa wa India kwa Afrika pakiwa na biashara baina ya nchi hizo inayofikia dola bilioni 8.6 kwa takwimu za mwaka 2024/25 pakiwa na miradi zaidi ya 700 ya wawekezaji kutoka India inayofikia uwekezaji wa dola bilioni tano iliyosajiliwa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania “ alisema Balozi Dey.
“Uhusiano wetu pia umebarikiwa na maono ya viongozi wetu, Waziri Mkuu wa India Narendra Modi alitembelea Tanzania mwaka 2016, Mwezi Oktoba mwaka 2023 Rais wa Tanzania, Samia Suluhu alitembelea India hii inaonyesha nia ya dhati ya viongozi hao kuboresha uhusiano baina ya nchi hizi mbili na maisha ya watu”
Soma zaidi habari hii kupitia Magazeti yetu (Nipashe, The Guardian) kesho....
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED