Watanzania milioni 6 wanategemea biashara ya mazao ya uvuvi

By Mwandishi Wetu , Nipashe Jumapili
Published at 08:12 AM Jul 06 2025
Uvuvi
PICHA: MTANDAO
Uvuvi

Rais Samia ameendelea kuimarisha biashara ya mazao ya uvuvi, ambapo thamani ya mauzo ya mazao hayo imeongezeka kutoka Sh bilioni 412 mwaka 2021 na kufikia Sh bilioni 675 mwaka 2024.

Ongezeko hilo linaenda sambamba na ongezeko la uzito kwa asilimia 64 kwa mazao yaliyouzwa kutoka tani 42,302 mwaka 2021 hadi tani 59,746 mwaka 2024.Hii imechangiwa na maboresho mbalimbali katika sekta ya uvuvi ambayo yameleta matokeo kama vile upatikanaji wa ajira za moja kwa moja kwa wavuvi 201,661 , wakuzaji viumbe maji 49,084 na takriban Watanzania milioni 6 wako katika shughuli mbalimbali zinazohusiana na uvuvi.

Katika kuongeza tija zaidi Serikali inaendelea na ujenzi wa mradi wa Bandari ya Uvuvi Kilwa Masoko wenye thamani ya Sh bilioni 279 ambao umefikia asilimia 81. Kukamilika kwa bandari hiyo kunatarajiwa kuzalisha ajira 30,000 na nchi kwa ujumla kunufaika na uvuvi wa bahari kuu.