Saudi Arabia yatangaza leo kuwa Sikukuu ya Eid Al-fitr

By Mwandishi Wetu , Nipashe Jumapili
Published at 12:05 PM Mar 30 2025
Saudi Arabia yatangaza leo kuwa Sikukuu ya Eid Al-fitr
Picha: Mtandao
Saudi Arabia yatangaza leo kuwa Sikukuu ya Eid Al-fitr

Saudi Arabia imetangaza kwamba Sikukuu ya Eid al-Fitr itaadhimishwa Jumapili, Machi 30, 2025, baada ya kuthibitishwa kuonekana kwa mwezi mwandamo wa Shawwal, mwezi wa kumi katika kalenda ya Kiislamu.

Nchi nyingine za Kiarabu, zikiwemo Falme za Kiarabu (UAE) na Qatar, pia zimethibitisha kuwa Eid al-Fitr itaadhimishwa siku hiyo hiyo.

Hata hivyo, nchi za Oman na Iran zimetangaza kwamba Eid al-Fitr kwao itaanza Jumatatu, Machi 31, 2025, baada ya wao kushindwa kuuona mwezi mwandamo katika maeneo yao.