WODI ya wazazi katika Hospitali ya Rufani ya Mkoa wa Temeke, Dar es Salaam, wamepokea msaada wa vitu mbalimbali, kwa wodi hiyo, pia kwa wauguzi na watoa huduma.
Akizungumza kwa niaba wafanyakazi wenzake, Ofisa Rasilimali Watu wa kampuni hiyo, Mariagoreth Mkenda, amesema msaada waliotoa ni kwa sababu ya kutambua thamani ya mama.
Pia, alisema wanatambua umuhimu wa sekta nzima ya afya kwa ujumla katika kipindi hiki cha siku ya wanawake dunia na kuwaomba wanawake wote kuwa na imani na wauguzi wanaowapatia matibabu mara wanapofika hospitalini hapo kupata matibabu,
Aye mmoja wa wazazi aliyejifungua katika hospitali hiyo, Zamoyoni Rashid, amewashukuru wanawake wa kampuni hiyo kwa kuwajali wanawake wenzao kwa kujitole msaada utakaowasaidia kutokana na baadhi yao hupungukiwa na vitu kutokana kosa pesa za kununu na kutokana na msaada huo walioupata kutoka Kisima Water utawasaidia sana,
Naye Kaimu Muuguzi Mkuu wa Hospitali hiyo, Beatrice Temba, amesema kwa niaba ya uongozi wa hospital hiyo wanatoa shukrani zao kwa wanawake wa Kampuni ya Kisima kwa kujitolea msaada wao kwa wanawake wenzao wanapata huduma hospitalini hapo
Amesema kuwa wanawake lazima tushikane mkono ili tuwe wazazi bora katika jamii.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED