RAIS wa mpito wa Gabon, Brice Clotaire Oligui Nguema, alikuwa wa kwanza kuwasilisha ombi lake siku ya Jumamosi asubuhi.
Aliongozana na mkewe Zita na umati mkubwa wa watu. Alitangaza kustaafu jeshini, sharti lililowekwa na kanuni za uchaguzi za Gabon kwa mwanajeshi kuwa na uwezo wa kugombea.
"Wizara ya Ulinzi ilikubali". Mkuu wa mpito atagombea kama mgmea huru na jukwaa lake jipya: chama cha za Wajenzi.
Waziri Mkuu wa zamani, Alain Claude Bilie By Nze, ambaye alikuwa hajaoneka katika siku za hivi karibuni, akizungukwa na wasaidizi wake, pia aliwasilisha ombi lake.
"Nitazungumza wiki ijayo," aliwaambia waandishi wa habari.
Wanaogombea pia ni mwanaharakati wa vyama vya wafanyakazi Jean Remy Yama, mwanaharakati wa mashirika ya kiraia nchii Gabon ambaye alikaa gerezani kwa miezi 18 chini ya utawala wa Ali Bongo, na Pierre Claver Maganga Moussavou, mwanzilishi wa chama cha PSD ambaye sasa ana umri wa miaka 72, ingawa kwa mujibu wa Katiba wagombea lazima wawe na umri wa miaka 35 na 70.
Maganga Moussavou tayari amewania urais mara nne.
Angalau wanawake wanne ni miongoni mwa wagombea. miongoni mwao: Zenaba Gniga Chaning na Marlène Essola Efoutamane, wote wagombea binafsi.
Mmoja wa wagombea wakuu ambao hawakukuwepo siku ya Jumamosi ni Albert Ondo Ossa, mgombea wa upinzani ambaye alijitenga na Ali Bongo mnamo mwaka 2023.
Maombi yote sasa yatachunguzwa kabla ya orodha rasmi ya wagombea kuchapishwa.
Hata hivyo wagombea kadhaa wameomba muda wa ziada kidogo, ili kupata hati ambazo hazipo, haswa risiti kutoka kwa Hazina inayothibitisha kwamba kweli wameweka amana ya faranga za CFA milioni 30.
RFI
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED