Hii hapa njia nyingine kupunguza tatizo la ajira nchini

By Halfani Chusi , Nipashe Jumapili
Published at 02:37 PM Jun 01 2025
Mwandishi wa Habari, Halfan Chusi akizungumza na Naibu Mkurugenzi wa Taasisi ya Goethe ofisini kwake
PICHA: HALFAN CHUSI
Mwandishi wa Habari, Halfan Chusi akizungumza na Naibu Mkurugenzi wa Taasisi ya Goethe ofisini kwake

TATIZO la ajira nchini limekuwa janga la taifa hii ni kutokana na kuongezeka kwa wasomi wanaomaliza vyuo kila kukicha.

Hata, hivyo kujifunza lugha ya kijerumani kunatajwa kuwa ni miongoni mwa njia zinazoweza kupunguza tatizo la ajira nchini.  Udadisi wa mwandishi wa habari hizi kwa waliojifunza kijerumani baada ya kumaliza chuo umebaini wengi wao wamepata ajira ndani na nje ya nchi.

Hii imetokana na lugha hiyo kutumika katika mataifa mengi na hivyo kufanya wote waliojifunza lugha hiyo kuwa katika soko la ajira.Kutokana na hali hiyo Nipashe ilifika katika moja ya taasisi inazofundisha na kusambaza lugha hiyo ya Goethe Institut ili kujua faida ugumu na wepesi kuyafikia mafanikio.

Naibu anasisitiza mtu anaposoma lugha ya kijerumani anajiweka katika soko la ajira na kwa asilimia kubwa na wengi waliosoma wameajiriwa. Nascov anasema pamoja na majukumu mengine ya ushrikiano katika utamaduni pia taasisi hiyo inatoa ufadhiri katika masuala mbalimbali ya utamaduni, wasanii kuimba, kuchora, ngoma za utamaduni na kushirikiana na balozi za nchi mbalimbali kwa kufanya makongano ya pamoja.
 
Nascov anazitaja faida kadhaa ambazo mtu anaweza akazipata akijifunza kijerumani na kwamba hiyo ndio kazi ya Goethe kusambaza ufundishwaji wa lugha ya kijerumani duniani. "Lugha ni sehemu utamaduni kwa mfano mzaramu anazungumza kizaramu kitu cha kwanza kinacho mtambulisha mtu ni lugha.

"Sasa tukirudi kwenye lugha ya kijerumani, ujerumani ni taifa lenye uvumbuzi wa aina mbalimbali kuanzia sayansi teknolojia kwahiyo kusoma kijerumani hakumfanyi mtu ajue kukiongea pekee hapana! atakutana na fursa nyingi kwa kuwa kijerumani ni lugha muhimu kwa wataalamu wanaotaka kufanya tafiti katika mambo mbalimbali ya kitaaluma.
 
"Faida za kukijua kijerumani kwa nchi ya ujerumani ngazi ya chuo kikuu kama mtu atakuwa amesoma kufikia daraja la juu kwa vyuo vya serikali anasoma bure hii ni fursa kwa watanzania. "Hii ni sehemu muhimu kwa sisi kusomesha mtoto sio kitu rahisi tunaona jinsi wazazi wanavyo beba mzigo mkubwa wanasoma mpaka elimu ya juu.
 
"lakini tunaona juhudi za serikali, nina maana katika kiwango kinacho kusanywa kwaajili ya kusadia watu kusoma chuo kwa mikopo kama watu wangehamasika kujifunza kijerumani watu wangeweza kwenda kujiendeleza kielimu bure ujerumani" anasema Nascov katika mahojiano na Nipashe ofisini kwake 
 
Anaendelea na ufafanuzi wake kwamba kwa mtu mwenye elimu ngazi ya Stashahada ujerumani wana utaratibu wanawapata fursa mbili atajifunza bure na utafanya kazi nusu ya muda wake. Kwa wenzetu wale hivyo vitu vinakwenda sambamba na anapewa fedha mwisho wa mwezi ninaona ni mfumo mzuri kwa vijana wa kitanzania kwa kujua tu kijerumani anaweza kupata fursa nyingi.
 
Nascov anasema mbali na elimu kwa sasa ujerumani ni nchi inayohitaji nguvu kazi kuna watu amabo tayari wameshahitimu kwetu wanaweza kupata fursa ya kwenda ujerumani wakafanya kazi kihalali kwa sababu tayari wanajua lugha yao.
 
Anasema mpaka sasa katika Chuo chao kilichopo Upanga mkoani Dar es Salaam wako wanafunzi wengi waliowafundisha kijerumani kutoka ndani na nje ya nchi pmoja na wageni kutoka nchi jirani za kameroon, Malawi, kongo, Zambia, na Burundi.

Anapoulizwa ni namna gani lugha hiyo inafundishwa anasema kijerumani kinafundishwa kwa kufuanta mfumo wa ufundishwaji lugha wa ulaya na kuna hatua sita ambazo mwanafunzi anapitia ambazo ni A1 A2 B1 B2 C1 C2. Anasema hatua hizo inategemeana na uhitaji wa mtu anavyoweza kujifunza lugha na inaweza kumchukua miezi tisa hadi 12 kukijua kijerumani.

OMBI LAKE SERIKALINI

Nascov anaiomba serikali iingize mtaala wa somo la kijerumani katika shule za sekondari kwa sababu taasisi yao haiwezi kuwafikia wengi japo wahitaji ni wengi. Anasema serikali ikiingiza hii lugha hiyo katika mitaala maana yake wanafunzi wataanza kuandaliwa kuanzia ngazi ya shule sekondari na watakapohitimu watakuwa na ujuzi wa lugha.
 
Anasema hukon nyuma waliwahi kushirikiana na serikali na mwaka 2009 walijaribu shule mbili kufundisha kijerumani ambazo ni sekondari ya Chang’ombe na zanaki tangu mwaka 2010 wananfunzi wengi walijifunza kijerumani katika shule hizo na hao wanaosoma somo hilo pia wanafanya vizuri katika masomo mengine tofauti.  
 
Anasema Sehemu ya kwanza ya wanafunzi waliomaliza katika shule hizo wako masomoni nchini Ujerumani wanasoma ‘masters’ wengine wameajiriwa sehemu mbalimbali ikiwamo ubalozi wa Ujerumani na wengine wanafanya kazi kama walimu na wengine wanajiendeleza.
 
Anasisitiza wanafunzi wengi wakijifunza lugha hiyo nchi inaweza, kupunguza tatizo la ajira kwa sababu inazungumzwa na watu milino 130 dunia na sio tu ujerumani kuna nchi tano zinatumia lugha rasmi. Nchi hizo ni pamopja Ujerumani, Austria, Ubelgiji, Uholanzi na Uswis.

“Shuleni kwetu huwa tunapokea wanafunzi 200 kwa kila msimu wa masomo na ada yake ni kuanzia Sh 700,000 hadi 1,100,000 kwa sasa tumepunguza ada ili watu waweze kumudu kufikia hatua hiyo ya B1 B2 ambayo inamwezesha mtu kupata sifa akiwa na taaluma aliyesomea kuajiriwa Ujerumani moja kwa moja” anasema 
 
Anasema tayari kwa mwaka huu si chini ya wanafunzi 600 wamepita katika mikono yao na walimu walionao shuleni ni watanzania na kwamba kitendo cha kutumia walimu wazawa kimesaidia kupunguza tatizo la ajira nchini.

Anasema pia wana mawasiliano na kampuni kubwa za utalii ambayo huomba wafanyakazi wake wafanyiwe mafunzo ili waweze kuzungumza na watalii kutoka ujerumnai wanpokuja nchini na kwamba kwa kufanya hivyo huongeza wigo wa wao kutembelea hifadhi zetu.

“Watalii wengi wa kijerumani wanapenda kongozwa na mtu anaeyejua kijerumani kwa sababu ndio njia pekee ya kuwavuta zaidi kuja nchini kwetu kutalii” anasema Nascov
 
Anasema wanaushirikiano na wa karibu na wizara za Utamaduni, Elimu na kwamba wiki mbili zilizopita walikwenda Zanzibar kwa Katibu Mkuu wa huko na amekubali wazo la lugha ya kijerumani kuingizwa katika mitaala ya elimu.

Pia anasema walikutana na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) kujadili namna gani kijerumani kinaweza kuingia katika mitaala ya elimu nchini. Hata hivyo, anasema mawazo ya wizara isiwe lugha ya kujifuzna kuanzia sekondari pekee bali wanapenda iwe kuanzia shule za msingi japo kwa sasa makubaliano yaliyopo waanzie sekondari baada ya hapo wataangalia namna ya kuanzia chini.

“Serikali inaunga mkono na wanachukulia hili kwa uzito mkubwa baadaye wataanza kutengeneza vitabu vinavyotokana na mawazo ya watanzania kwa lugha ya kijerumani. “Baada ya kupata mafunzo hayo muhitimu naweza kufanya maombi ya kazi ujerumani lakini uzuri uliopo kuna taasisi ya ujerumani inataanza kazi muda siyo mrefu itakuwa mahusi kwaajili ya kuwasaidia Watanzania kwenda nchini huko kwa masuala mbalimbali kama kubadilishana utamaduni na kuongeza ujuzi katika mambo mbalimbali.

MNUFAIKA ANENA 

Julius Kileo, ni moja kati ya wanufaika wengi waliojifunza kijerumani kupitia taasisi ya goethe akiwa katika Shule ya Sekondari Chango’mbe anasema amepata faida kubwa kutokana na kujifunza lugha hiyo na kwa sasa anafanya kazi kama mwalimu anafundisha lugha hiyo na ni jambo lililobadili miasha yake kiujumla.

Kileo anasema mwanzoni wakati anajifunza lugha hiyo hakuamini kama siku moja anaweza kubadili maisha yake bali alijifunza kwa kuwa alipenda kukijua kijerumani lakini anashangaa mafanikio makubwa aliyo yapata kwa sasa. 

Anasema hakuwa na ugumu kujifunza lakini changamoto katika sekondari hiyo aliyosoma hakukua na kipindi kamili cha masomo hayo hivyo walikosa muda mwingi wa kujifunza kwa nafasi.

“Ninashauri serikali iweke nafasi ya kutosha wanafunzi kujifunza lugha za kigeni ili kufungua milango ya biashara na ajira niwatake wanafunzi walio hitimu vyuo mbalimbali wajifunze lugha ya kijerumani watapata fursa nyingi sana.
 
“Serikali ishirikiane na Taasisi ya Goethe kuipa nguvu, watu wengi watambue kama wanatoa mafunzo hayo kwakuwa watakao jua lugha hiyo watakuwa katika nafasi ya kuajiriwa na kupunguza tatizo la ajira nchini” anasema kileo katika mahojiano na nipashe kuelezea faida alizopata kujifunza kijerumani kupitia taasisi hiyo.