Bodi ya EWURA yaridhishwa na uendelezaji wa miradi ya umeme wa Jotoardhi

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 05:03 PM Dec 11 2024
Bodi ya EWURA yaridhishwa na uendelezaji wa miradi ya umeme wa Jotoardhi.

Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imeonesha kuridhishwa na hatua zilizofikiwa katika uendelezaji wa miradi ya kuzalisha umeme wa jotoardhi kwenye maeneo ya Ngozi (MW 70) na Kyejo-Mbaka (MW 60) mkoani Mbeya.

Ziara hiyo, inayoongozwa na Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Prof. Mark Mwandosya imelenga kuona hatua iliyofikiwa katika uendelezaji wa miradi hiyo muhimu ya kimkakati.

Akizungumza  baada ya kutembelea mradi huo , Prof. Mwandosya amesisitiza umuhimu wa kupanua wigo wa vyanzo vya kuzalisha umeme ikiwamo jotoardhi ili kuboresha upatikanaji wa huduma za nishati kwa wananchi. 

Aidha, Prof. Mwandosya ameipongeza Kampuni ya Maendeleo ya Jotoardhi Tanzania (TGDC) kwa juhudi zake za kuhakikisha miradi hiyo inasonga mbele.

Naye, Kaimu Mkurugenzi wa Umeme wa EWURA,  Mhandisi Aurea Bigirwamungu,  amesisitiza dhamira ya kushirikiana na wadau wote kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa mafanikio.

1