Hali ya utulivu yarudi Nairobi baada ya maandamano

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 05:03 PM Jun 28 2024
Askari jeshi ambae akilinda doria katika viunga vya mji wa Nairobi kufuatia maandamano ya wananchi.
Picha: Daniel Irungu/EPA
Askari jeshi ambae akilinda doria katika viunga vya mji wa Nairobi kufuatia maandamano ya wananchi.

HALI ya utulivu imeanza kurudi katika mji mkuu wa Kenya na maeneo mengine nchini Kenya kufuatia maandamano ya kupinga ongezeko la kodi na ushuru.

Biashara na maduka yamefunguliwa huku wananchi wakiripotiwa kuendelea na shughuli zao za kawaida.  

Maandamano hayo yaliyoongozwa na vijana yalizuka wiki hii baada ya bunge la kitaifa kuupitisha mswada tata wa fedha uliotoa mapendekezo ya kuongeza ushuru.

Kufuatia maandamano hay Rais wa Kenya William Ruto alisema hatoutia saini mswada huo wa fedha na kutaka ufanyiwe marekebisho.