WAASI wa M23 jana Januari 29 wameendelea na mashambulizi baada ya kuuteka Mji wa Goma huku wakielekea Bukavu Mji mkuu wa jimbo la Kivu Kusini, katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Vikosi vya M23 vimeonekana vikielekea kusini kutoka mji wa Minova, upande wa magharibi wa Ziwa Kivu, kulingana na vyanzo vitano vya kidiplomasia na usalama, mmoja wao alikuwa akiwasiliana moja kwa moja na waasi.
Kasi ya kundi hilo kuendelea na mashambulizi na kuikalia miji ya hiyo likielekea kusini inatajwa endapo watadhibiti eneo itakuwa ni mara ya kwanza kudhibitiwa na kundi lolote la waasi tangu kumalizika kwa vita vikuu vya Kongo miaka 20 iliyopita.
Hata hivyo katika njia hiyo M23 wanakabiliwa na upinzani mkubwa kutoka kwa Jeshi la Burundi lililotumwa nchini humo kuimarisha ulinzi likiwa katika eneo la Kavumba ulipo uwanja wa ndege wa Mji huo eneo ambalo ni lazima waasi hao wapiti ili kufika Bukavu.
Kusonga mbele kuelekea Bukavu kunakuja wakati M23 ikiimarisha ngome yake mpya huko Goma, mji mkuu wa Kivu Kaskazini na kitovu cha watu waliokimbia makazi yao, wafanyakazi wa misaada, walinda amani wa Umoja wa Mataifa na vikosi vya Kongo.
Majimbo yote ya Kivu Kaskazini na Kivu Kusini yana migodi mingi ya madini, na mapambano ya kudhibiti rasilimali nyingi za Kongo ni mojawapo ya vichochezi vya vita mashariki mwa nchi hiyo kubwa.
Rasilimali hizo pia ni pamoja na coltan, ambayo hutumiwa katika simu mahiri, laptop na komputa
Licha ya msururu wa shughuli za kidiplomasia, ikiwa ni pamoja na Marekani kuiambia Rwanda "imefadhaishwa sana" na kuanguka kwa Goma kwa wapiganaji wa M23, kulikuwa na dalili zinazoongezeka waasi kuchukua udhibiti wa jiji hilo.
Milio ya risasi ndizo kelele pekee zilizosikika katika baadhi ya wilaya za pembezoni mwa jiji la kando ya ziwa lenye wakazi zaidi ya milioni mbili ambapo waasi wa Jumatatu walivamia.
Miili ya watu imeshuhudiwa ikiwa imelala mitaani, hospitali zikiwa zimezidiwa na walinda amani wa Umoja wa Mataifa wakijikinga katika kambi.
Leo hii vikosi vya serikali ya Kongo havikuonekana katikati ya jiji hatua iliyowapa nafasi wapiganaji wa M23 kuonekana wakifanya doria kwenye mpaka na Rwanda na kukata minyororo na kufuli ambazo zilikuwa zimezuia njia kwa watembea kwa miguu na magari.
Kundi la M23 ndilo kundi la hivi karibuni linaloongozwa na Watutsi wanaotajwa kuungwa mkono na Rwanda kushambulia Kongo tangu kutokea kwa mauaji ya halaiki nchini Rwanda miaka 30 iliyopita.
Wakati Wahutu wenye itikadi kali walipowaua Watutsi na Wahutu wenye msimamo wa wastani, na kisha kupinduliwa na majeshi yanayoongozwa na Watutsi yakiongozwa na Kagame. .
Hivi karibuni Rais wa Rwanda, Paul Kagame amesema baadhi ya wahalifu waliotimuliwa wamejihifadhi nchini Kongo tangu mauaji ya halaiki, na hivyo kuwa tishio kwa Watutsi wa Kongo na Rwanda yenyewe.
Kongo inakataa malalamiko ya Rwanda, na inasema Rwanda imetumia wanamgambo wake kupora madini ya faida kubwa nchini humo.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED