Nusu ya Wasudan wana uhaba wa chakula

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 05:43 PM Jun 28 2024
Wasudan wakiwa katika msururu wa kupokea misaada ya kiutu.
Picha: Guy Peterson/AFP
Wasudan wakiwa katika msururu wa kupokea misaada ya kiutu.

UMOJA wa Mataifa umetahadharisha kuwa takriban watu milioni 26 nchini Sudan wanakabiliwa na viwango vya hatari vya uhaba wa chakula.

Mashirika ya Umoja wa Mataifa ya UNICEF, lile la chakula na kilimo FAO na la mpango wa chakula duniani WFP yamesema katika taarifa ya pamoja kuwa, nusu ya raia wa Sudan wanakabiliwa na changamoto ya kulisha familia zao.

Kwa mujibu wa ripoti iliyoandaliwa kwa kutumia kipimo cha kuboresha tathmini ya usalama wa upatikanaji wa chakula na mchakato wa kupitisha maamuzi, IPC, kuna hatari kubwa ya maeneo 14 nchini humo kukumbwa na baa la njaa iwapo vita kati ya jeshi na kundi la wanamgambo la RSF vitaaendelea.

IPC imeorodhesha maeneo ya mji mkuu Khartoum, Darfur, Kordofan na jimbo la El Gezira kama maeneo ambayo yanakabiliwa na changamoto ya uhakika wa kupata chakula.

 DW