Dk. Yonazi: Watanzania tumieni fursa sabasaba kujifunza

By Maulid Mmbaga , Nipashe
Published at 11:41 AM Jul 06 2024
Dk. Jim Yonazi, Katibu Mkuu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu katika maonyesho ya 48 ya biashara ya kimataifa maarufu Sabasaba jana, Dar es Salaam.
Picha: Maulid Mmbaga
Dk. Jim Yonazi, Katibu Mkuu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu katika maonyesho ya 48 ya biashara ya kimataifa maarufu Sabasaba jana, Dar es Salaam.

KATIBU Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dk. Jim Yonazi ametoa wito kwa wananchi kutumia maonyesho ya sabasaba kama fursa ya kujifunza masuala mbalimbali ikiwemo yanayohusu kazi zinazofanywa na ofisi ya waziri mkuu.

Akizunhumza leo mkoani Dar es Salaama, katika maonyesho ya 48 ya biashara ya kimataifa maarufu Sabasaba, Dk. Yonazi amesema wanachokifanya katika maonyesho hayo ni pamoja na kueendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu masuala mbalimbali ya uratibu.

Amesema ofisi ya waziri mkuu imejipanga kuhakikisha inaendelea kuwafikia wananchi wanaopata huduma katika banda jumuishi la ofisi hiyo wakati wa maonesho hayo kwa kuhakikisha wanapewa elimu juu ya masuala mbalimbali yanayohusu ofisi hiyo pamoja na taasisi zilizochini yake.

"Niwasisitize wananchi wayaone maonyesho haya kama fursa kubwa kwao kwani taasisi nyingi ziko hapa kwaajili ya kutoa elimu ya kina juu ya masuala mbalimbali ambayo ni muhimu mwananchi wa kawaida kuwa na uelewa nayo," alisema Dk. Yonazi. 

Aidha, Dk. Yonazi ametumia nafasi hiyo kutoa wito kwa wananchi na wadau mbalimbali kuendelea kutembelea banda hilo na kupongeza namna watumishi wa ofisi hiyo wanavyoendelea huwahudumia wananchi na wadau wanaofika huku akiwasihi watumishi hao kuendelea kuzingatia weledi zaidi katika utoaji huduma na elimu kwa umma.