Kongamano la wafanyabiasha kuwavuta wawekezaji nchini

By Faustine Feliciane , Nipashe
Published at 07:53 PM Jul 01 2024
Mwenyekiti wa Chama cha watoa huduma za kifedha kwa njia ya mtandao (TAFINA), Cynthia Ponera.
Picha: Mpigapicha Wetu
Mwenyekiti wa Chama cha watoa huduma za kifedha kwa njia ya mtandao (TAFINA), Cynthia Ponera.

KONGAMANO kubwa la wafanyabiashara Afrika Mashariki “East Africa Investment Forum’ linatarajiwa kufanyika kwa siku mbili Septemba 12-13 jijini Dar es Salaam na kuvuta wawekezaji mbalimbali.

Akizungumza jana, Mwenyekiti wa Chama cha watoa huduma za kifedha kwa njia ya mtandao (TAFINA), Cynthia Ponera, alisema kongamano hilo kubwa lina lengo la kuunganisha wafanyabisahara hususani watoa huduma za kifedha kwa njia ya mtandao kutoka nchi za Afrika Mashariki na Kati.

Alisema, katika uandaaji wa kongamano hilo, wamepata ushirikiano mkubwa kutoka Benki Kuu ya Tanzania ambao nao watashiriki.

“Tunafuraha sana kuandaa kongamano hili kubwa, lengo letu ni kuona wawekezaji na wadau tunaenda pamoja, kongamano hilo litatachochea kwa kiasi kikubwa ushirikiano katika uwekezaji,” alisema Cynthia na kuongeza,

“Hapa nchini tunatarajia wanachama wetu, kampuni 62 zitashiriki, laikini pia tunatarajia washiriki kutoka nchi za Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, tunaamini kongamano hili litasaidia kuwaleta wawekezaji watakaongalia fursa za uwekezaji hapa nchini,” alisema Cynthia.