ATCL, Via Aviation wasaini mkataba wa ushirikiano

By Vitus Audax , Nipashe
Published at 11:27 PM Jul 03 2024
ATCL, Via Aviation wasaini mkataba wa ushirikiano
Picha: Vitus Audax
ATCL, Via Aviation wasaini mkataba wa ushirikiano

SHIRIKA la Ndege Tanzania (ATCL) imesaini mkataba wa ushirikiano na kampuni ya huduma kwa wateja ya Via Aviation kwaaajili ya kuhudumia wasafiri wa daraja ya biashara kupitia jengo lake la Serengeti Lounge lilipo katika Uwanja wa Ndege wa Mkoa wa Mwanza.

Akizungumza leo Julai, 3, 2024 wakati wa utiaji saini Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Ladislaus Matindi amesema lengo la kusaini mkataba na Via Aviation kutumia jengo la Serengeti ni kuhakisha wateja wa daraja la biashara la Gold pamoja na wateja wa kudumu wa shirika hilo wanapata huduma nzuri sambamba na kupata maeneo ya mapumbuziko huku wakiendelea na shughuli zao.

Akizungumza ya  kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Via Aviation, Susan Mashibe, Mkuu wa Usimamizi na Uendelevu wa kampuni hiyo, Caleb Takayindisa amesema lengo la kuanzisha huduma hiyo ni kuboresha viwango vya ubora wa usafirishaji katika viwanja vya ndage nchini.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Said  Mtanda ameyataka mashirika hayo kuhakikisha wanaongeza ubora wa huduma kwa wateja ili huduma zao ziwe na tija katika Mkoa wa Mwanza na Taifa kwa ujumla.

“Gharama zenu pia ziwe rafiki ili kwa wateja mnao wapokea waeze kurejea tena na tena. Pia jitahidi kufanya kwa ushindani kwani ujenzi wa jengo la abiria la kimataifa ukikamilika napo litakuwepo jengo la namna hiyo hivyo hakikisheni lenu linakuwa na huduma zitakazowarejesha kwenu wateja amesema mtanda.

Kwa mujibu wa Meneja wa huduma kwa wateja katika jengo hilo la Serengeti wanatoa huduma za bure kwa wateja wa daraja la biashara wa ndege za ATCL zikiwemo vinywaji laini na pombe, usaidizi wa mizigo, Internet ya bure, gari la kubeba wateja, kushughulikia ukaguzi pamoja na usaidizi wa mizigo.