Makalla amtaka Mbowe ajiandae kujiuzulu

By Romana Mallya , Nipashe
Published at 02:24 PM Jul 06 2024
Katibu wa NEC - Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Amos Makalla, akizungumza na wanaCCM leo katika ukumbi wa Diamond Jubilee, mkoani Dar es Salaam.
PICHA: Romana Mallya
Katibu wa NEC - Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Amos Makalla, akizungumza na wanaCCM leo katika ukumbi wa Diamond Jubilee, mkoani Dar es Salaam.

Katibu wa NEC - Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Amos Makalla, amemtaka Mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, ajiandae kujiuzulu.

Makalla ambaye ni mlezi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam ametoa kauli hiyo leo katika ukumbi wa Diamond Jubilee, wakati akizungumza na wanachama wa chama hicho ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara ya siku saba mkoani Dar es Salaam.

Akihutubia katika mkutano huo, Makalla amesema amesikia Mbowe akisema lazima wachukue ushindi wa majimbo ya Kaskazini yote na akishindwa atajiuzulu.

"Sasa nasi tumwambie na  tumemrekodi kuwa ajiandae kutoka maana sisi tutachukua majimbo yote ya Kaskazini na Tanzania yote, sisi sio wabaguzi tunapiga kote, sio yeye anabagua ninajua anajiandaa na uwenyeketi," amesema.

Makalla amesema vyama vya upinzani vimekosa mvuto na mwelekeo na ndio maana watu wao wanazidi kuhamia CCM.

"Hapa kuna Diwani wa CHADEMA ataka kuja nimpokee na bado tutapiga bomu lingine mpaka wakimbiane," amesema Makalla.

Mkutano huo umehudhuriwa na maelfu ya wanachama wa chama hicho.