Uamuzi wa serikali kutoa vibali vya uagizaji kulishusha bei ya sukari

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 10:33 PM Jul 05 2024
Mkurugenzi wa Bodi ya Sukari Tanzania (SBT), Profesa Kenneth Bengesi,
Picha: Mpigapicha Wetu
Mkurugenzi wa Bodi ya Sukari Tanzania (SBT), Profesa Kenneth Bengesi,

Uamuzi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoa vibali vya uagizaji wa sukari kwa kampuni nyingine za wafanyabiashara kulichangia kushusha bei ya sukari kwa kiasi kikubwa hali iliyoleta ahueni kubwa kwa wananchi.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Bodi ya Sukari Tanzania (SBT), Profesa Kenneth Bengesi, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo mchana jijini Dar es Salaam.

“Ingawa kampuni hizi za wafanyabiashara zinadhihakiwa kuwa ni za vocha, hizi ndio kampuni zilizoingiza sukari nchini kwa haraka katika kipindi kigumu cha upungufu mkubwa na kuifanya bei ya sukari ishuke,” alisema Profesa Bengesi.

1

Taarifa iliyotolewa na Bodi ya Sukari Tanzania inaonyesha Kampuni za wafanya biashara zillifanikisha kuingizwa kwa sukari nyingi nchini ndani ya muda mfupi ikilinganishwa na kampuni za wazalishaji.

Ongezeko hilo lilifanikisha kushusha bei sukari nchini kutoka wastani wa Sh 7000 mwezi Februari hadi Sh 2800 mwezi Juni.

Bodi ya Sukari iliamua kutolea ufafanuzi hoja za upotoshaji zilizotolewa na wadau wa sukari nchini Tanzania, kwa nia ya kuondoa hofu kwa wananchi na Watanzania kwa ujumla.
2