Musoma Vijijini wachangamkia mikopo ya uvuvi wa vizimba

By Sabato Kasika , Nipashe
Published at 03:39 PM Aug 21 2024
Musoma Vijijini wamachamkia mikopo ya uvuvi wa vizimba.
Picha:Mpigapicha Wetu
Musoma Vijijini wamachamkia mikopo ya uvuvi wa vizimba.

WAVUVI wa Musoma Vijijini mkoani Mara, wamechukua mkopo nafuu usio na riba kutoka serikalini ili kuweka vizimba vya samaki ndani ya Ziwa Victoria.

Miongoni mwao ni Chama cha Ushirika cha Wavuvi wa kitongoji cha Busumi kilichochukua mkopo wa Sh. milioni 117.

Mbunge wa Musoma Vijijini Profesa Sospeter Muhongo, ambaye pia anahamasisha wananchi kuchangamkia fursa hiyo amesema chama hicho kina wanachama 20.

"Hao wamepata mkopo ili kununua vizimba vinne, vifaranga vya samaki, chakula na bima ya ufugaji wao wa samaki," amesema Prof. Muhongo.

Amefafanua kuwa wataalam wa kusuka vizimba  wamekamilisha kazi ya kusuka vizimba, na kwamba tayari vimeshapelekwa ndani ya Ziwa Victoria eneo la Kijiji cha Suguti.

1
"Uvuvi wa vizimba kwa upande wa jimbo la Musoma Vijijini, umeanza kwa mafanikio hasa maeneo ya vijiji vya Kigera (Etuma), Bwai Kwitururu na Suguti," amesema.

Ameongeza kuwa, wavuvi wa maeneo mengine wanazidi kuhamasika na wanajitayarisha kutuma maombi ya mkopo serikalini ili wanunue vizimba.

"Wavuvi wa Musoma Vijijini wanaishukuru serikali yetu chini cha uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia mikopo ambayo haina riba, na pia kwa kuboresha uvuvi wao kwa kuufanya kuwa kisasa na wenye mapato makubwa.

2