Nondo asisitiza umuhimu wa katiba imara

By Maulid Mmbaga , Nipashe
Published at 08:14 PM Aug 21 2024
MWENYEKITI wa Ngome ya Vijana wa ACT Wazalendo Abdul Nondo.
Picha: Mpigapicha Wetu
MWENYEKITI wa Ngome ya Vijana wa ACT Wazalendo Abdul Nondo.

MWENYEKITI wa Ngome ya Vijana wa ACT Wazalendo Abdul Nondo amesisitiza umuhimu wa kuwa na katiba imara na yenye nguvu kama sehemu ya kuchochea maendeleo ya Tanzania na kukuza ufanisi wa kitaasisi

Ameyasema hayo leo katika mkutano ulilofanyika mkoani Dar es Salaama na kukutanisha baraza la vyama vya siasa nchini, kwaajili ya kutoa maoni kuhusu dura mpya ya maendeleo ya mwaka 2050.
 
"Katiba ndio msingi mkubwa kabisa utakaokuja kuleta maendeleo haya tunayoyazungumza, katiba italeta utaasisi na utawala wa sheria. Tumeona tumepata viongozi ambao wanafanya maamuzi ya hovyo kiasi cha kukimbiza wawekezaji. Tuweke misingi imara ambayo itatuletea uchumi imara," amesema Nondo.
 
Pia ameshauri kuwa kuelekea 2050, ni muhimu kwa serikali kuongeza kasi katika urasimishaji wa shughuli zisizo rasmi kwakuwawezesha mitaji na kutengeneza mazingira mazuri kwa ajira ambazo bado hazijaingia kwenye mifumo iliyo rasmi.
 
Nondo pia ameitaka serikali kuhusianisha na kufungamanisha kilimo na viwanda kwa kuwa na viwanda vya kuongeza thamani maeneo mbalimbali kulingana na asili ya kilimo kinacholimwa kwenye maeneo husika ili kusaidia wananchi kunufaika nacho.