'CHADEMA bado wanayo nafasi kutia saini kanuni za maadili'

By Enock Charles , Nipashe Jumapili
Published at 11:43 AM Jun 22 2025
Ado November
PICHA: MTANDAO
Ado November

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeelezwa kuwa bado kina nafasi ya kutia saini kanuni za maadili ya uchaguzi ili kipate fursa ya kushiriki uchaguzi.

Akizungumza katika Kongamano la Sheria lililofanyika jijini Dar es Salaam jana, Ado November kutoka Chama cha Wanasheria wa Serikali alisema chama hicho kinayo fursa hiyo.

Kanuni hizo tayari zilishatiwa saini na Vyama 18 vya Siasa nchini isipokuwa CHADEMA pekee ambao walitaka kufanyika mabadiliko kwanza ili kutia saini. “Leo CHADEMA wakija wakitaka kushiriki nafasi wanayo ‘as long as’ hatujafikia hatua ya kuanza mchakato wa uchaguzi”.alisema Ado