Waumini kanisa la Gwajima wakusanyika tena

By Enock Charles , Nipashe Jumapili
Published at 01:08 PM Jun 22 2025
Waumini wa Ufufuo na Uzima
PICHA: MTANDAO
Waumini wa Ufufuo na Uzima

Ikiwa ni Jumapili nyingine leo waumini wa Kanisa la Ufufuo la Uzima linaloongozwa na Mchungaji, Josephat Gwajima wamekusanyika kusali pembeni ya barabara.

Jeshi la polisi nchini lilitangaza kulifungia kanisa hilo mwezi uliopita na kisha kuwakamata waumini waliojitokeza kwa ibada katika Jumapili zilizofuatia wakidaiwa kukaidi agizo la jeshi hilo. Waumini hao leo wamefika kanisani hapo asubuhi na kuanza kuimba nyimbo, kisha kuomba na kutoa sadaka kabla ya baadae polisi kujitokeza na kufanya mazungumzo na mmoja ya wachungaji wa kanisa hilo ambaye baada ya hapo alitoa tangazo la kuwatawanya waumini hao.