Marekani imeishambulia maeneo ya nyuklia ya Iran kwa makombora ya B-2 , amesema Ofisa wa Marekani.
Rais wa Marekani Donald Trump anasema Marekani imekamilisha mashambulizi kwenye maeneo matatu ya nyuklia nchini Iran, ikiwa ni pamoja na Fordo, Natanz na Esfahan.
Fordo 'imeenda', aliandika Trump kwenye ujumbe wake kwenye mtandao jukwaa la ujasusi la kijamii.
"Tumekamilisha shambulio letu lililofanikiwa sana kwenye maeneo matatu ya Nyuklia nchini Iran, ikiwa ni pamoja na Fordow, Natanz, na Esfahan. Ndege zote sasa ziko nje ya anga ya Iran," aliandika kwenye Truth Social.
Trump aliongeza kuwa "mzigo kamili wa mabomu" ulirushwa Fordo na ndege zote zilikuwa njiani kurudi Marekani.
Ndege za kivita za Marekani B-2 ambazo ndizo zenye uwezo pekee wa kupiga makombora kwenye kufikia maeneo ya nyuklia ya Iran yalipo chini ya ardhi, awali yaliripotiwawalikuwa wameripotiwa kuhamishiwa katika eneo la kisiwa cha Marekani cha Guam, na kusababisha uvumi kwamba ndege hiyo inaweza kuhusika katika shambulio la Marekani dhidi ya Iran.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED