Wafanyakazi wa ndege huwa na majukumu mengi. Anaweza kuanza kwa kuhudumia chakula hadi kushika maiti wakati abiria anapofariki ndege ikiwa angani.
Ikiwa abiria atafariki wakati ndege iko angani, wafanyakazi wa ndege lazima wachukue hatua za haraka.
"Kuanzia kuwahudumia abiria kama kawaida hadi kulazimika kutunza miili yao, wanapopoteza maisha. Bila kusahau kudhibiti umati," alisema Jay Robert, mmoja wa wafanyakazi wa ndege mwenye umri wa miaka 40.
"Ubongo lazima ufanye kazi mara mbili. Kwa upande mmoja, bado tunapaswa kuandaa kifungua kinywa au chakula cha jioni kwa abiria 300. Wakati huo huo, pia tunapaswa kukabiliana na kifo.
"Utafiti uliochapishwa katika jarida la New England Journal of Medicine mwaka 2013 ulihitimisha kwamba vifo kwenye ndege ni tukio la "nadra." Lakini hutokea. Utafiti huo uliangalia simu za dharura kutoka kwa mashirika matano ya ndege kwenda vituo vya mawasiliano vya matibabu kati ya Januari 2008 na Oktoba 2010.
Ni 0.3% pekee ya wagonjwa wanaopata dharura za matibabu kwenye safari za ndege hufa, kulingana na utafiti.
Mwezi uliopita, wanandoa wa Australia Mitchell Ring na Jennifer Colin walielezea uzoefu "wa kutisha" wa kukaa karibu na mwili wa mwanamke kwenye ndege kutoka Melbourne hadi Doha.
Wafanyakazi wa ndege waliuweka mwili wa mwanamke huyo kwenye blanketi karibu na Ring kwa saa nne bila kujitolea kuusogeza.
Qatar Airways ilisema kuwa imefuata miongozo ifaayo na kuomba radhi kwa "usumbufu au huzuni yoyote ambayo tukio hili linaweza kusababisha", kwa abiria wengine.
CHANZO: BBC
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED