Wasira ahoji aliko Mbowe

By Enock Charles , Nipashe Jumapili
Published at 01:10 PM Mar 23 2025
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) bara, Steven Wasira
PICHA: MTANDAO
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) bara, Steven Wasira

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) bara, Steven Wasira amehoji alipo Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe huku akidai huenda bado anauguza majeraha ya uchaguzi.

Akizungumza na wanachama wa CCM mkoani Kagera, Wasira alidai uchaguzi wa ndani ya chama uliofanywa na CHADEMA Mwezi Januari mwaka huu umekiacha chama hicho katika hali ya sintofahamu na migawanyiko ya ndani.

“Chadema wamemtukana Mbowe mpaka amepotea yaani kumbe matusi yanaweza kumfanya mtu akapotea, Mbowe hajulikani aliko, haonekani na si kwamba amefariki yuko lakini bado anauguza madonda” amesema Steven Wasira.