Tume ya uchaguzi yaongeza siku mbili uandikishaji Dar

By Halfani Chusi , Nipashe Jumapili
Published at 06:48 PM Mar 23 2025
Wananchi mkoani Dar es Salaam wakijiandikisha
Picha: Halfan Chusi
Wananchi mkoani Dar es Salaam wakijiandikisha

TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza kuongeza siku mbili zaidi za uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapigakura, mkoani Dar es Salaam na sasa litatamatika Machi 25, 2025.

Hatua hiyo imetangazwa na Mwenyekiti wa INEC, Jaji wa Mahakama ya Rufani, Jacobs Mwambegele, leo, Machi 23, 2025 baada ya mwitikio mkubwa wa wananchi wa mkoani humo, kujitokeza kwa wingi katika yzaidi tangu Machi 17 na ulitarajiwa kukamilika leo, Machi 23, mwaka huu.

“Hivyo basi, napenda kuwatangazia wananchi wote wa mkoa wa Dar es Salaam kuwa, Tume imeongeza siku mbili za uboreshaji wa Daftari kwa tarehe 24 na 25 Machi, 2025 na zoezi litakamilika tarehe 25 Machi, 2025 saa 12:00 jioni,” amesema Jaji Mwambegele.