RAIS Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania imeridhia kuanza maandalizi ya kuwa mwenyeji wa shindano la Miss World Mwaka 2027
Uamuzi huo unatajwa kufungua mafanikio lukuki kwa nchini, ikiwamo katika uendelezaji wa vipaji, sanaa na utalii na kukuza chapa ya nchi katika dunia iliyosheheni ushindani.Rais Samia Suluhu Hassan, kwenye kikao hicho“Ukiondoa matukio ya awali yanayokwenda mwaka mzima, fainali pekee ya shindano hilo, ambayo huhudhuriwa na takribani watu 5,000 ukumbini.Dk. Hassan Abbasi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili“Tukio hilo kubwa duniani husomwa, hutazamwa na kufuatiliwa na watu zaidi ya bilioni diniani,” amesema Dk. Hassan Abbasi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili, mara baada ya kikao hicho muhimu, akifafanua namna utalii utakavyonufaika.