Harambee Stars yajigamba kuicharaza Zambia leo

By Mwandishi Wetu , Nipashe Jumapili
Published at 01:17 PM Aug 17 2025
Timu ya Taifa ya Kenya
Picha: Mtandao
Timu ya Taifa ya Kenya

KOCHA wa Timu ya Taifa ya Kenya Benni McCarthy, amezungumza juu ya ni kwa nini lazima waicharaze Zambia katika mechi yao ya mwisho ya Kundi A leo Jumapili kwenye michuano ya CHAN 2024.

"Tulijiwekea malengo mwanzoni mwa mashindano, lakini kila mtu aliamini kuwa hatuwezi. Tuliambiwa tuko kwenye "Kundi la Kufa", lakini baada ya michezo mitatu, tumejikuta tukiongoza kundi. Tunataka kufurahiya kucheza mpira wetu, na kumaliza mechi za makundi tukiwa juu,"

"Jumapili, ni mchezo ambao ni lazima tushinde, hatuzingatii kufuzu kwa sababu tayari tumefuzu, ni katika hali tu ya kumaliza kampeni nzuri ambayo tayari tumekuwa nayo na ninawaambia wachezaji ili wawe bora zaidi, unahitaji kushinda walio wazuri zaidi, na nadhani tayari tumethibitisha hilo katika hatua zote za mechi ya makundi na Dr Congo, Angola na Morocco."

Kenya alianza kampeni yao kwa mtindo wa aina yake, ikishinda Dr Congo bao 1-0 kwenye mechi ya ufunguzi kabla ya kupambana kweli kweli na kutoka sare ya 1-1 dhidi ya Angola kwenye mechi ya pili ya makundi.

Katika mechi yao ya tatu, waliishangaza Morocco kwa ushindi wa 1-0, na kuwa kifua mbele katika Kundi A wakiwa na pointi saba.

Chanzo: BBC