Nigeria yaishinda Morocco na kutwaa taji la WAFCON 2024

By Mwandishi Wetu , Nipashe Jumapili
Published at 05:57 PM Jul 27 2025
Wachejzaji wa timu ya wanawake ya taifa Nigeria
Picha: BBC
Wachejzaji wa timu ya wanawake ya taifa Nigeria

NIGERIA imeibuka na ushindi wa aina yake kipindi cha pili kwa kuwazaragaza wenyeji Morocco mabao 3-2 na kuweka rekodi ya kuibuka kidedea kwenye taji la 10 katika Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (Wafcon) 2024.

Atlas Lionesses waliongoza kwa mabao 2-0 wakati wa mapumziko mjini Rabat kupitia kwa Ghizlane Chebbak kutokana na shuti maridadi kabisa la Sanaa Mssoudy.

Lakini Esther Okoronkwo aliwatia moyo Waafrika Magharibi baada ya kipindi cha mapumziko, na kukomboa bao kwa mkwaju wa penalti dakika ya 64 baada ya Nouhaila Benzina kuwahi krosi ya Folamide Ijamilusi.

Okoronkwo aliingia ndani ya eneo la Morocco na kumuonyesha kivumbi Ijamilusi aliposawazisha katika dakika ya 71, kisha akamtumia mchezaji wa akiba Jennifer Echegini kufunga bao la ushindi zikiwa zimesalia dakika mbili mchezo kumalizika.

Uwanja wenye uwezo wa kuingia watu 21,000 ulikumbwa na ukimya huku wachezaji wa Super Falcons wakijigaragaza uwanjani kwa mbwembwe wakati wanasherehekea kipenga cha mwisho kilipopigwa baada ya kuibuka washindi tukio ambalo litasalia kwenye kumbukumbu za wengi kwa muda mrefu.

Nigeria ilitangaza kampeni yao kama Mission X na wamefikia lengo lao kwa kutwaa tena taji waliloshinda mara ya mwisho mwaka wa 2018 na kuhifadhi rekodi yao kwa 100% katika fainali za Wafcon.

Wakati huo huo, Morocco ilikuwa imeajiri kocha aliyeshinda Kombe la Dunia la Wanawake 2023, Jorge Vilda katika harakati za kutwaa taji lao la kwanza la bara, lakini sasa wamepoteza fainali mfululizo za Wafcon.

Chanzo: BBC