Tanzia: Baba mzazi wa Samatta afariki dunia

By Mwandishi Wetu , Nipashe Jumapili
Published at 02:27 PM Jul 06 2025
news
Picha Mtandao
Mzee Ally Samatta

Huzuni kubwa imetanda katika familia ya nahodha wa timu ya taifa Tanzania ‘Taifa Stars’ Mbwana Samatta kutokana na taarifa za kifo cha Baba yake mzazi Ally Samatta.

Taarifa za awali zimeeleza kuwa mzee Samatta amefariki alifajiri ya leo akiwa nyumbani kwake huko Mbagala mkoani Dar es Salaam, na taarifa hizo zimethibitishwa na mwanae, Mohamed Samatta.

Hata hivyo, kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa ndugu wa familia Mzee Ally Samatta alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya kiafya.

Aidha, enzi za uhai wake Mzee Samatta aliwahi kuichezea timu ya taifa akivaa jezi namba 10.