Wakulima watakiwa kujitokeza 77 kupata mikopo ya pembejeo

By Mary Geofrey , Nipashe
Published at 03:57 PM Jul 02 2024
Meneja Mkuu wa Biashara wa benki hiyo, Leah Ayoub.
Picha: Mpigapicha Wetu
Meneja Mkuu wa Biashara wa benki hiyo, Leah Ayoub.

WAKULIMA wametakiwa kujitokeza katika maonyesho ya Kimataifa ya Biashara (sabsaba) kwaajili ya kupata fursa za mikopo ya pembejeo za kilimo kutoka Benki ya Equit.

Rai hiyo imetolewa leo na Meneja Mkuu wa Biashara wa benki hiyo, Leah Ayoub, wakati akizungumza na waandishi wa habari wakati wakizindua banda lao katika viwanja hivyo.

Amesema wanatoa mikopo ya pembejeo, mitaji ya wakulima na wameshatoa Sh. bilioni 46 katika mazao ya mahindi, pamba na alizeti.

Amesema wamejikita pia katika kukopesha wakulima na wajasiriamali wadogo.

Leah amesema pia wametoa mikopo ya mitaji kwaajili ya kuendesha biashara na kununua na kuuza bidhaa.

1

Amesema pia wanatoa mikopo kwaajili ya ujenzi, kununua nyumba na gari.

Amesema pia wateja wanaonunua na kusambaza bidhaa za viwanda na kumkopesha baada ya kujiridhisha na utoaji huduma hiyo.

"Wateja wetu waje kwenye banda letu hapa sabasaba na maeneo mbalimbali nchini ili kupata huduma tunazotoa ikiwamo huduma ya bima wanazotoa," amesema.

2