Asasi ya Family Vibes kukabilina na chuki

By Imani Nathaniel , Nipashe
Published at 05:32 PM Jul 04 2024
Mchungaji Eliona Kimaro.
Picha: Imani Nathaniel
Mchungaji Eliona Kimaro.

Family Vibes Foundation imewaalika wadau mbalimbali wa maendeleo kushiriki katika harambee ya kuwezesha uzindizi wa mpango wa kukabiliana na chuki ulimwenguni.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi  Mtendaji wa Taasisi hiyo Dk. Mayrose Majinge amesema kuwa  lengo la programu hiyo watu wapate utulivu pamoja na amani kama inavyosifika nchi ya Tanzania kuwa ndio kisiwa cha amani.

Amesema wataalamu wa saikolojia wamegundua kwamba katika ulimwenguni wa sawa chuki ni gonjwa la kuambukiza na lenye sumu hatari na kuenea kwa kazi sana na kuuwa zaidi ya magonjwa mengine.

Dk. Maryrose amesema kuwa uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika Septemba mwaka huu katika falme za kiarabu Abu Dhabi ambao unatqrajiwa kuwa na thamani ya sh.bilioni mbili.

Lengo kuu la program hiyo ni kujenga uelewa , kuhamasisha na kushirikisha jamii kutambua athari za chuki na kuweza kushiriki kazi ya uzuiaji kwa kuchukua hatua stahiki za kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazosababisha chuki katika maisha ya kila siku ikiwa ni pamoja na kuachana, kuharibu mahusiano, ujinga, umaskini, magonjwa, vita na vifo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Dk. Mayrose Majinge.
"Nchi yetu ya Tanzania kama zilivyo jamii zote ulimwenguni inakabiliwa na ugonjwa hatari wa chuki na hivyo kusababisha maasi mengi kuongezeka na utu kupotea " 

Kwa kuwa chuki imetambulika kuwa ugonjwa hatari sana wa kuambukiza na kuenea kwa kazi na kuua kuliko ugonjwa mwingine katika kizazi hiki,sisi families vibes kwa kushirikiana na wadau wa nchi za falme ya kiarabu tumeona umuhimu wa kuanzisha program hii ili kusaidia ulimwenguni kukabiliana na chuki" alisema.

Kwa upande wake kiongozi wa dini Mchungaji Eliona Kimaro , alimpongeza Dk. Maryrose kwa kuanzisha programu hiyo ya kukabiliana na maswala ya chuki.

"Viongozi wa dini tunajitahidi sana kuwahusia waumini wetu kwenye nyumba za ibada hasa kuachana na tatizo la chuki.

"Ikumbukwe chuki ilianza katika familia ya adamu na hawa kwa kizazi cha kwanza ambapo mmoja alimuonea wivu mwenzake na kujaa chuki akasababisha kifo na yeye kuwa mwendawazimu" alisema.