Silaa: Msinifuate Dodoma, jitokezeni kwenye kliniki za ardhi maeneo yenu

By Julieth Mkireri , Nipashe
Published at 06:45 PM Jul 04 2024
WAZIRI wa Ardhi,Nyumba na Maendelo ya Makazi Jerry Silaa
Picha: Mpigapicha Wetu
WAZIRI wa Ardhi,Nyumba na Maendelo ya Makazi Jerry Silaa

WAZIRI wa Ardhi,Nyumba na Maendelo ya Makazi Jerry Silaa amesema wananchi wanatakiwa kujitokeza kwenye kliniki za ardhi zilizopo katika maeneo yao badala ya kumfuata katika ofisini Dodoma na Dar es Salam.

Ametoa kauli hiyo alipokuwa akizindua kliniki ya ardhi maarufu kama Samia kliniki kwa ajili ya kusikiliza migogoro ya ardhi katika Wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani.

Amesema wananchi wanaopeleka migogoro yao katika ofisi yake jijini Dodoma ni ngumu kumkuta kwani muda mwingi anakuwa kwenye maeneo ya migogoro kusikiliza migogoro na kutafutia ufumbuzi.

"Natangaza hapa na nilishasema kwenye maeneo mengi wananchi wwnye migigoro mkija ofusini Dodoma au Dar es Salam ni ngumu kunikuta na ni nadra sana kunikuta na wataalamu wa mkoa wa Pwani na mikoa mingine," amesema.

Waziri Silaa amesema wananchi wanatakiwa kutumia kliniki zilizoanzishwa kwenye maeneo yao kwani huko atakuwepo Waziri au mbadala wake kutoka ofisi yake ambaye ataambatana na wataalamu wa ardhi ngazi ya mkoa na Halmashauri.

Pia amesema katika ofisi ya ardhi watendaji aanatakiwa wajumuike pamoja kuwasilikiza wananchi wenye migogoro na kutoa suluhu ya haraka.

"Ningependa ofisi ya ardhi wataalamu wapatikane wote sehemu moja, masuala ya ardhi sio ya kujificha kama kwa daktari, mumpokee mwananchi mwenye malalamko asikilizwe na utatuzi upatikane," amesema.

Kadhalika Waziri Silaa amepongeza Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Halima Okash kwa namna anavyoshuvhulikia migogoro ya ardhi.

Silaa amesema kitendo anachofanya Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo kusikiliza migogoro ya ardhi akiwa na wataalamu wa ardhi itasaidia kumaliza kabisa migogoro hiyo katika Wilaya yake.

Waziri huyo amesema mbali ya Mkuu huyo wa Wilaya kufanya kliniki kwenye eneo lake pia amekuwa akitafuta suluhu kwa kukutanisha pande zenye mgogoro.