WAZIRI Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, atakutana na Rais wa Marekani Donald Trump katika Ikulu ya White House wiki ijayo.
Ofisi ya Netanyahu imesema ziara hiyo itafanyika Februari 04, 2025 na kwamba anakuwa kiongozi wa kwanza wa kigeni kualikwa katika Ikulu ya White House wakati wa muhula wa pili wa Trump.
Afisa wa Ikulu ya White House alithibitisha kwamba kutakuwa na mkutano mapema wiki ijayo, lakini akasema tarehe na wakati bado havijahitimishwa, kwa mujibu wa mshirika wa BBC wa Marekani CBS News.
Akizungumza na waandishi wa habari siku ya Jumatatu, Trump alisema Netanyahu atasafiri kwenda Washington kukutana naye "hivi karibuni sana", lakini kutoa tarehe maalum.
BBC
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED