CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimetoa mapendekezo matatu kwa serikali kufuatia uamuzi wa Rais wa Marekani,Donald Trump kusitisha misaada kwa sekta ya afya.
Kwa mujibu wa taarifa kwa umma iliyotolewa (Januari 28,2025), na Mwenyekiti wa Kamati ya Afya na Maendeleo ya Jamii ya Bunge la Wananchi CHADEMA, Ashura Masoud, lazima hatua zichukuliwe kukabili mabadiliko hayo.
Chama hicho kimependekeza serikali kuandaa mkakati wa dharura wa kisera na kibajeti wa kuhakikisha inakuwa na fedha za kutosha kwenye Mfuko wa Kudhibiti UKIMWI na Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI kwa kubana matumizi na kutenga vyanzo maalum na vya lazima katika bajeti ya taifa,ili kupunguza makali ya uhaba wa fedha za ARVs na UKIMWI.
Pia Bunge linaloendelea sasa kujadili ajenda ya dharura,serikali iwasilishe taarifa ya tathimini na mkakati wa kina wa namna ya kukabiliana na upungufu wa fedha katika sekta ya afya na nyingine za maendeleo,kisha litokea na azimio.
Pia Rais Samia Suluhu Hassan na wakuu wenzake wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Umoja wa Afrika (AU) wafanye mkutano kwa ajili ya kutafuta ufumbuzi mpana na wa kina zaidi kupata vyanzo mbadala vya fedha na kuziba pengo la kibajeti linalosababishwa na Marekani kusitisha misaada ya maendeleo.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo,uamuzi wa Rais Trump kusitisha misaada ya maendeleo ya nje ya Marekani na kujitoa kwenye Shirika la Afya Duniani (WHO) kunaweza kusababisha athari kubwa katika sekta ya afya hususan dawa za ARVs ya kupunguza makali ya VVU,na mapambo dhidi ya kuenea VVU na UKIMWI.
Amesema takwimu zinaonesja kuwa asilimia 90 ya fedha zinazotumika katika eneo hilo ni kitoka nje ambapo Mpango wa Dunia wa Rais wa Marekani wa kukabiliana na UKIMWI (PEPFAR) unachanhia asilimia 40 katika kapu hilo na michango ya mashirika mengine kama WHO,Kituo cha Kudhibiti Magonjwa cha Marekani (CDC) na Global Fund.
"Idadi ya waathirka wa VVU hadi sasa wanaonufaika na misaada ni tajribani mil 1.5,na wastani wa Sh.bilioni 204 kwa mwezi hutumika,"amesema.
Aidha,amesema: " Tathimini iliyofanywa na Kamati ya Afya ya Bunge la Wananchi imebaini kusitishwa kwa misaada hii kutaathiri huduma ya ARVs pamoja na mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI KWA asilimia 50.".
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED