MNH miongoni vituo tiba majaribio selimundu

By Christina Mwakangale , Nipashe
Published at 04:42 PM Feb 19 2025
MNH miongoni vituo tiba majaribio selimundu
Picha: MNH
MNH miongoni vituo tiba majaribio selimundu

HOSPITALI ya Taifa Muhimbili (MNH), inatarajiwa kuwa miongoni mwa vituo vitakavyoshiriki majaribio ya dawa mpya ya selimundu kwa wagonjwa wanaohudumiwa hospitalini hapo.

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mafunzo, Utafiti na Ushauri wa Kitaalam, Dk. Robert Moshiro, alisema majaribio hayo yatawahusisha baadhi ya wagonjwa wa selimundu, ili kubaini ufanisi wa dawa hiyo mpya.

MNH miongoni vituo tiba majaribio selimundu
Alisema hatua hiyo inakuja baada ya kauli iliyotolewa na kukutana na wageni kutoka Taasisi ya Clinical Trials Africa Network (CTAN), walifika kuangalia iwapo MNH inafaa kuwa kituo cha majaribio hayo.