Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika, amesema chama chake kitajifungia kwa wiki moja pamoja na viongozi wapya na wastaafu ili kuandaa mkakati wa pamoja kuelekea uchaguzi.
Mnyika aliyasema hayo leo mkoani Dar es Salaam wakati wa kumkabidhi ofisi rasmi Mwenyekiti mpya wa CHADEMA, Tundu Lissu.
"Uongozi huu ni wa awamu ya saba na ni mpya, lazima tupate muda wa kupanga mipango. Kesho tutajifungia na viongozi wakuu wote, wastaafu na wapya, kwa pamoja. Tutatoka na mwelekeo mpya na kuanza kuzunguka kuendesha mapambano katika taifa letu," amesema Mnyika.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED