NLD yazindua kampeni, walaani wanufaika wa TASAF kufanyishwa kazi ngumu

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 08:51 PM Nov 21 2024
Katibu Mkuu wa Chama cha The Nation League For Democracy (NLD),Doyo Hassan Doyo , akizungumza na Wakazi wa Kijiji cha Kwedikwazu wilayani Handeni mkoani Tanga, wakati wa uzinduzi wa kampeni za Uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 27.
PICHA: BONIFACE GIDEON
Katibu Mkuu wa Chama cha The Nation League For Democracy (NLD),Doyo Hassan Doyo , akizungumza na Wakazi wa Kijiji cha Kwedikwazu wilayani Handeni mkoani Tanga, wakati wa uzinduzi wa kampeni za Uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 27.

CHAMA cha The Nation League For Democracy (NLD) hatimaye kimezindua rasmi kampeni zake kuelekea Uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 27 mwaka huu, huku kikija na agenda lukuki ambazo zitasaidia kuongeza wigo wa ajira na maendeleo na kulaani vikali serikali kuwatumikisha kazi ngumu ikiwemo kuchimba mitaro,visima na mabwawa kwa wanachama wa TASAF.

Uzinduzi wa kampeni zake zimefanyika katika Kijijij cha Kwedikwazu wilayani Handeni,ambapo chama hicho kimesimamisha wagombea kwa sehemu kubwa ya Vijiji na mitaa Wilayani humo,  Akizungumza na Wakazi wa Wilaya hiyo,Katibu Mkuu wa NLD, Doyo Hassan Doyo amesema,chama hicho kimesimamisha wagombea kwenye mitaa na vijiji zaidi ya 700 n nchini na kinatarajia kupata ushindi katika maeneo yote yenye Wagombea,

"Chama chetu kimesimamisha wagombea kwenye mitaa na vijiji vingi nchini,kwa kwa Kijiji hiki tumesimamisha wagombea kwenye mitaa yote na wajumbe,pia Wilaya yetu tumesimamisha wagombea kwenye mitaa na vijiji karibu maeneo yote,tunatarajia kuchukua ushindi katika maeneo yote yenye Wagombea wetu,kwani tumesimamisha wagombea wanaokubalika katika jamii na wenye sifa njema na mfano wa kuigwa katika jamii,hivyo hatuoni sababu yakutokushinda" alisisitiza Doyo

Doyo alisema katika Kijijiji hicho kinategemewa kwa uzalishaji wa madini lakini kwenye akaunti ya kijiji hicho hakuna pesa. "Kijiji hiki kina madini lakini kwenye akaunti ya kijiji hakuna hata mia mbovu,maana yake uongozi uliokuwepo madarakani umeshindwa kusimamia maslahi ya wakazi wa kijiji hiki,sisi NLD tukiingia madarakani tutahakikisha kijijiji hiki kinapata mapato kutokana na madini ,tutajenga ofisi nzuri ya kijiji pamoja na madarasa mazuri yakusomea" alisisitiza

Kuhusu kutumikishwa kazi ngumu kwa wanufaika wa TASAF, Doyo alidai serikali imekuwa na tabia yakuwatumikisha wanachama wa TASAF kufanya kazi ngumu na kuahidi  kuwalipia kila mzee Sh.30,000 kila mwezi bila kufanya kazi ngumu.

"Serikali yetu imekuwa ikiwatumikisha kazi ngumu wazee wanaopata fedha za TASAF,wanachimba mabwawa,kuchimba mitaro, visima nk, lakini pia kwenye Wanachama wa TASAF wamo vijana Wenye umri mdogo,kitu ambacho ni kinyume na malengo ya mpango wa TASAF, lengo  la TASAF nikusaidia Kaya Maskini hususani wazee, lakini wazee hao ndo wanatumikishwa kazi ngumu,nipo tayari kuwalipia elfu 30 kila mwezi kwakila  Mzee katika Kijijiji hiki endapo tutashinda Uenyekiti" aliongeza Doyo