TANAPA yatoa milioni 20 kwa ajili ya uokoaji Kariakoo

By Imani Nathaniel , Nipashe
Published at 05:57 PM Nov 21 2024
Kamishna wa TANAPA Musa Kuji (kulia) akimkabidhi Katibu Mkuu Jim Yonazi hundi ya milioni 20 kusaidia uokoaji wa janga la ghorofa lililoporomoka Kariakoo, Dar es Salaam. Kushoto ni Jenerali Mstaafu George Waitara.
Picha: Imani Nathaniel
Kamishna wa TANAPA Musa Kuji (kulia) akimkabidhi Katibu Mkuu Jim Yonazi hundi ya milioni 20 kusaidia uokoaji wa janga la ghorofa lililoporomoka Kariakoo, Dar es Salaam. Kushoto ni Jenerali Mstaafu George Waitara.

Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) limeichangia Milioni 20 kwa ajili ya shughuli ya uokozi katika jengo lililoporomoka hivi karibuni Mtaa wa Mchikichi na Kongo Kariakoo jijini Dar es Salaam.

1Msaada huo umekabidhiwa mapema leo na Mwenyekiti wa Bodi ya TANAPA Mkuu wa Majeshi mstaafu, Jenarali George Waitara alipotembelea eneo la tukio.

 Wakati wa kukabidhi msaada huo Jenarali Waitara amesema kuwa msaada huo ni kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za uokoaji unaoendelea pamaja na utamaduni wa Watanzania wakusaidiana pindi yanapotokea majanga.

“Panapotokea maafa kama yaliyotokea umekuwa utamaduni wetu watanzania kusaidiana, inasikitisha sana jengo hilo kuporomoka na kusababisha maafa makubwa na vifo” amesema.

“TANAPA ni sehemu moja wapo ya wananchi wa Tanzania tumeguswa tukaona na sisi tutoe chochote kama msaada wa kuendelea na shighuli za uokoaji, kuhudumia waathirika na shughuli nyingine kama ambavyo watanznaia wenzetu wengine walivyotoa msaada” ameongeza.